Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na kibao chake cha ‘Demu sio’,
msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khalid Tunda ‘Tunda Man’ ameachia
kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Riziki’.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es
salaam, Tunda alisema wimbo huo unaelimisha jamii hivyo amewataka mashabiki wa
kazi zake wakipokee kibao hicho kwa miwili.
Alisema wimbo huo unaujumbe mzito katika jamii
na anaomba mashabiki wake waendelee kumpa sapoti katika kazi zake ambapo
amejipanga kutoa burudani iliyoenda shule kwa mashabiki wake.
“Naomba mashabiki wangu waendelee kunipa sapoti
katika kazi zangu kwani nimejipanga kuelimisha jamii inayonizunguka kwa kutumia
kipaji changu, hivyo wakae mkao wa kula,” alisema Tunda.
Mbali na kutokana kibao hicho, Tunda Man
lishawahi kutamba na vibao vyake kama, Goma la Manzese, Hali mbaya, na
nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya
redio.
No comments:
Post a Comment