Ronaldo akishangilia moja ya bao lake
Sergio Ramos akiwa mgongioni kwa Ronaldo wakishangilia bao la uongozi
Wachezaji wa Barca chini ya nahodha Carles Puyol wakilalamikia moja ya maamuzi ya refa
Lionel Messi kulia na Cesc Fabregas kushoto wakiwa hawaamini kama ngoma imekula kwao Nou Camp
Rafael Varane akiifungia Madrid bao la tatu kwa kichwa, akiwazidi kupaa mabeki wa FC Barcelona
Hapa Gerard Pique akimwangusha chini Ronaldo na kusababisha Madrid kupewa penati
Ronaldo kulia akifunga mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kuangushwa chini na Pique
Hapa Ronaldo 'aki-slide' kushangilia bao la pili aliloifungia Madrid
Kocha Jose Mourinho akimkumbatia Rafael Varane baada ya kuifungia Madrid
BARCELONA,
Hispania
Beki Jordi Alba akaifungia bao la kufutia machozi Barca
katika dakika ya 89, lakini halikutosha kuiepushia kichapo hicho, na kujikuta
wenyeji hao wakikubali kufungwa nyumbani mabao matatu na Madrid kwa mara ya kwanza tangu Machi 2007
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo usiku ya juzi alifunga mara
mbili kuipa Real Madrid ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya FC Bracelona, katika
mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Mfalme ‘King's Cup.’
Pambano hilo lilipigwa ndani
ya dimba la Nou Camp jijini hapa, ambapo kwa ushindi huo sasa Madrid
ilikuwa ikisubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Atletico Madrid na Sevilla, ili
kujua mpinzani wake wa fainali ya michuano hiyo itakayopigwa Mei.
Ronaldo, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga
katika mechi sita mfululizo za mahasimu hao 'El Clasicos' akiwa ugenini, wakati
alipotikisa nyavu kwa kwa mkwaju wa penati dakika ya 13 baada ya yeye mwenyewe
kuangushwa na Gerard Pique.
Licha ya bao hilo,
Barca iliendelea kumiliki mpira, huku Ronaldo akibaki kuwa mtu hatari pekee
katika kikosi hicho, akifumua na kukosa mashuti kadhaa, kabla ya kufunga kwa mpira
uliorudi ‘rebound’ ya Angel Di Maria dakika ya 57.
Ronaldo, ambaye amekuwa akilaumiwa kwa kushindwa kung’ara
katika mechi muhimu, hilo likawa bao lake la 12
katika mechi 18 alizoicheza dhidi ya Barca tangu alipojiunga Madrid mwaka 2009 na ni mara yake ya pili
kufunga mara mbili akiwa Nou Camp.
Madrid ikatia chumvi katika
donda la mechi ya awali wakati Raphael Varane, ambaye aliisawazishia Madrid katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bao 1-1
kwenye dimba la Santiago Bernabeu, – alipounganisha kona nyavuni dakika ya 68
kuipa Madrid
bao la tatu.
Beki Jordi Alba akaifungia bao la kufutia machozi Barca
katika dakika ya 89, lakini halikutosha kuiepushia kichapo hicho, na kujikuta
wenyeji hao wakikubali kufungwa nyumbani mabao matatu na Madrid kwa mara ya kwanza tangu sare ya 3-3 Machi
2007.
SuperSport.com
No comments:
Post a Comment