Meneja wa Kinywaji cha Redd's Victoria Kimaro akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency na Mratibu wa shindano la Urembo la Redds Miss Tanzania 2013, Hashim Lundenga ameishukuru jamii kwa kuyaunga mkono mashindano hayo hali inayopelekea ubora na kuongezea heshima Taifa.
Lundenga
alisema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akiongea na wandishi wa habari
juu ya mwelekeo wa mashindano hilo hatua ya awali ya Vitongoji na Wilaya ambazo
zinatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi Mei.
“Napenda
kuchukua fursa hii kuwajulisha wadau wa sanaa ya urembo, kuwa hatua ya ngazi ya vitongoji na wilaya yalishaanza kwa
nchi nzima na tayari baadhi ya maeneo wamshamaliza
mashindano hayo na maeneo
mengine yakitarajia kumaliza mwisho wa mwezi huu, tunashukuru kwa kuyapokea”
alisema Lundenga.
Na kuongeza
kuwa, kutokana na muamko huo, kwa mwaka huu kutakuwa na mikoa 24, inayofanya
mashindano hayo, ambapo kuna Kanda 11,Vyuo
vya Elimu ya juu 17, Wilaya 18, huku vituo vya Mkoa wa Dar e Salaam vikiwa 11,
vyote kwa pamoja vinafanya idadi ya vituo zaidi ya 80.
Kwa hatua
hiyo, Lundenga alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ya awali,
Mashindano ya Kanda yataanza katikati ya mwezi Juni na kuingia katika hatua
inayofuata.
Kwa hatua hiyo
pia, Lundenga aliwashukuru wazazi na walezi ambao wamewaruhusu watoto zao
wasichana kujitojkeza kwa wingi katika ushiriki wa shindano hilo.
Kwa upande
wake, Meneja wa Kinywaji cha Redd’s Original , Victoria Kimaro alisema kupitia
kinywaji chao bora hapa nchini cha Redds, kimedhamiria kuhakikisha mashindano
hayo yanaendelea kuwepo kwa ubora na kuendelea kutoa udhamini kwa ngazi zote.
“Tumeendelea
kutoa udhamini katika ngazi mbalimbali kuanzia kitongozi hadi Kitaifa, hivyo ili mashindano kuwa bora ni vyema
warembo wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili kunogesha na kuongeza ushindani nah
ii italeta mapinduzi makubwa katika tasnia hii ya urembo” alisema Kimaro.
Aidha Kimaro aliwaomba wadau kuendelea kukiunga mkono kinywaji hicho ili kuweza kupata
nguvu ya kuwaletea burudani.
Fainali hizo zitakazofanyika siku ya Ijumaa Mei 17 katika sehemu mbalimbali ikiwemo Redds Miss
Moshi Mjini, Redds Miss Kibaha,Redds Chuo cha Ustawi wa Jamii, Redds Miss
Ubungo, na Redds Miss Mzizima.
No comments:
Post a Comment