Na
Elizabeth John
WASANII
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’
anatarajia kuachia ngoma yake mpya hivi karibuni inayokwenda kwa jina la
'Maisha ya Skongo'.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana Dogo janja alisema katika ngoma hiyo ameshirikiana na
msanii wa muziki huo Pancras Ndaki 'PNC'.
Alisema
yuko katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho, ambacho anaamini
kitakonga nyoyo za mashabiki wa muziki huo ndani na nje ya nchi.
"Namshukuru
mungu kazi zangu huwa zinapokewa vizuri na mashabiki wangu, kitu ambacho kinanipa
moyo wa kuendelea kufanya vizuri katika 'game' hivyo nawaomba mashabiki wa kazi
zangu waendelee kusubiri vitu vizuri kutoka kwangu,"alisema Dogo Janja.
Aliongeza
kuwa ameamua kumshirikisha PNC katika kazi hiyo kutokana na uwezo wake katika
tasnia ya muziki, ikiwa ni pamoja na historia yake nzuri ya kuutangaza muziki
wa Bongo.
No comments:
Post a Comment