Elizabeth John
MKALI
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sunday Mangu 'Linex', anatarajia kusambaza
ngoma yake mpya hivi karibuni inayokwenda kwa jina la 'Kimugina'.
Linex,
kwa sasa anatamba na kazi yake ya 'Mahakama ya Mapenzi' mbali na kuwa na kazi
nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya
redio.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Linex alisema wimbo huo anatarajia
kuutambulisha hivi karibuni katika vituo mbalimbali vya redio na kwamba tayari
upokatika hatua za mwisho za kukamilika.
Alisema
wimbo huo ni miongoni mwa vibao vyake ambavyo ameviandaa kwa ajili ya mashabiki
wake, hivyo wakae mkao wa kula kuipokea kazi hiyo.
"Kila
wimbo ninaoutoa lazima kunakuwa na kisa cha kweli nyuma yake, hivyo kuna baadhi
ya maneno yaliyoko humo ni ya kweli na mengine ni stori tu, ambazo nimeamua
kuwapa mashabiki wangu," alisema Linex.
No comments:
Post a Comment