Na
Mwandishi wetu, Tanga
MWANADADA
anayetamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Mwasiti Almas
amewataka vijana kujiunga na mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili
kujihakikishia usalama wa maisha bora kutokana na fursa zilizopo kwenye mifuko hiyo kwasasa.
Akizungumza
juzi katika viwanja vya Tangamano mjini hapa, msanii huyo alisema kwasasa
vijana ndio nguvu kazi ya taifinayotegemewa, lakini kukosa uelewa wa kuzitumia
fursa zilizopo zimesababisha wengi kuwa tegemezi katika familia zao na mzigo
kwa taifa.
“Mtanzania
wa kawaida kama unataka mitaji ya uhakika, ingia kwenye mfuko wa NSSF kani
mfuko huo umetusaidia sana sisi tumetupa mwangaza mkubwa wa maendeleo,”
alisema.
Msanii
wa hip hop, Niki wa Pili alisema vijana wengi wamekosa taarifa sahihi kuhusu
namna ya kutumia fursa zilizopo katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa
ujumla hali inayowafanya waonekane ni tegemezi.
“Tatizo
ni jinsi tunavyowaandaa vijana kwani elimu wanayoipata haiendani na mazingira
ya fursa yaliyopo kwenye maeneo yao, utaona kijana toka anapata elimu ya msingi
hadi chuo hakuna kitu cha ujasiriamali alichojifunza wala taarifa zozote kuhusu
kujitegemea alizozipata,” alisema.
Alisema ifike wakati vijana walioko shuleni wasiishie
kupata elimu ya darasani bali waandaliwe kwaajili ya kuhakikisha wanapewa na
elimu nyingine ya fursa zilizopo kwenye eneo husika walipo.
Naye
Mwakilishi wa NSSF Makao Makuu, Salim Kimaro alisema mfuko huo kwasasa
umejikita katika kuwasaidia vijana kiuchumi kwa kuwakopesha mikopo, ambayo
wataitumia kuendesha biashara zao walizobuni.
“Chamsingi
ni vijana kujiunga katika vikundi na kuanzisha vyama vya akiba na mikopo SACCOS,
baada ya hapo wawe mwanachama wa mfuko wetu na wawe wamechangia kwa kipindi cha
miezi sita watapata fursa ya kukopeshwa fedha,” alisema Kimaro.



No comments:
Post a Comment