HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 10, 2013

RAIS KIKWETE AZINDUA SHULE YA SEKONDARI
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasikiliza kwa makini wanafunzi wa kidato cha tano wanaosoma Shule ya Sekondari ya Miono Wilayani Bagamoyo, Nyekwabi Jackline George,Penina Odara na Magret Machinyita wakitoa maelezo ya jaribio la sayani somo la biolojia wakati Rais alipofungua rasmi shule hiyo jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua maktaba ya Shule ya Sekondari ya miono Muda mfupi baada ya kuizindua shule hiyo jana Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuizindua rasmi shule ya sekondari ya Miono iliyopo Wilayani Bagamoyo,Jana.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoa wa Pwani.
Mtafiti katika kituo cha Ifakara Health Institute tawi la Bagamoyo Dkt.Annete Tumbo akitoa maelezo kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete juu ya maendeleo ya tafiti mbalimbali ikiwemo chanjo ya ugonjwa wa Malaria.Rais Kikwete alitembelea kituo hicho jana. (Picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment

Pages