NA KENNETH
NGELESI, MBEYA
BARAZA la umoja wa
vijana wa Chama cha Mapinduzi (Uvccm), Mkoa wa Mbeya, leo (Julai 5)wanatarajia
kufanya mkutano wa mwaka, sanjari na shughuli ya kuapishwa kwa makamanda 11 wa
umoja huo katika ngazi ya Mkoa na Wilaya.
Umoja huo
umebadilisha utaratibu wa awali wa kuwa kuwasimika badala yake
watakuwa wakila kiapo ambapo kwa mkoa wa Mbeya ndo umeanza.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana katika ofisini za umoja huo, Mwenyekiti wa
Uv-ccm mkoa, Aman Kajuna, alisema mkutano huo wa mwaka wa kikanuni
utakuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo kujadili changamoto ndani ya chama.
Kajuna alisema kuwa
mgeni rasmi katika mkutano huo utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Mkapa, Jijini hapa, atakuwa ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na ushirika,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi.
Alisema miongoni mwa
mambo yatakayojadiliwa ndani ya mkutano huo ni kuweka mikakjati na
kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika
mwaka huu.
“Kwa kweli licha ya
kuwa na mikakati ya uchaguzi wa serikali za mitaa, pia tutajadili
changamoto za uchaguzi Mkuu ujao, ikiwemo mikakati ya kurejesha jimbo la Mbeya
mjini tulilowaazima hawa wenzetu” alisema Kajuna.
Akifafanua zaidi
Kajuna alisema CCM inauhakika wa kulikomboa jimbo hilo kutokana na
ukweli kuwa mbunge aliyepo ameonekana kupwaya.
Jimbo la Mbeya mjini
linaongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia mbunge
wake, Joseph Mbilinyi , aliyemshinda mgombea wa CCM, Benson Mpesya,
ambaye ambaye alibwagwa katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Kwa upande wake
katibu wa Umoja huo, Said Yasin, alisema baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa
baraza, siku itakayofuata ya Julai 6 kutakuwa na shughuli ya
kusimikwa kwa makamanda 11 wa umoja huo katika ngazi ya mkoa na Wilaya.
Alisema atakayefanya
shughuli ya kuwasimika makamanda hao ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Taifa ,
Jerry Silaa, itakayofanyika katika viwanmja vya Ruanda Nzovwe.
Aliwataja makada wa
chama hicho watakaosimikwa kuwa ni kamanda wa umoja huo ngazi ya
Mkoa kuwa ni Yona Sonelo, anayefanya shughuli zake Jijini Dar es salaam.
Mak amanda wengine
na Wilaya zao kwenye mabano kuwa ni Philipo Mulugo (Chunya), Tonebu
Chaula (Mbeya Mjini), Oran Njeza (Mbeya Vijijini).
wengine
watakao apishwa Ibrahmu Mwakabwanga (Mbarali), Ibrahm Mwanjilinji (Mbozi),
Richard Kasesela (Rungwe), Elius Asangalwisye (Kyela), Twaha Kalabeba (Momba)
na Gidion Cheyo (Ileje).






No comments:
Post a Comment