Na Keneth Ngelesi, Mbeya
UONGOZi wa timu ya soka ya Mbeya City inayoshiriliki ligi
kuu Tanzania bara ya kutoka Mbeya
umesema kuwa licha ya kuingia mtakaba wa Binsulumu kudhamini timu hiyo lakini
bado inahitaji mchango wa kila hali kutokana na kiwango hicho kuto kidhi
mahitaji yote ya timu hiyo.
Akizungumza na wachama wa timu hiyo tawi la Sido katika
hafla ya kuipongeza timu hiyo kwa kufanya vizuri katika msimu uliopita na
kuukaribisha msimu mpya iliyo andaliwa
na tawi hilo na kilifanyika katika Hotel Gr jiji hapa katibu huyo alisema fedha
hizo kitapunguza ukali wa mahitaji.
Hata hivyo Katibu alifikia hatua ya kutoa hilo baada ya
mashabiki hao kuhoji uongozi huo kwamba mara ya kwanza mashabiki walikuwa
wanajisafirisha kwa fedha zao kwenda na timu hiyo sasa uongozi huo hauoni haja
ya kuchangia nauli kwa mashabiki kutokana na kuanza kupata wadhamini?
Akifafanunua zaidi
Kimbe alisema kuwa uendeshaji wa ni ghama kubwa kwani kwa msimu uliopita jumla
ya shilingi milioni 800 zilitumika hivyo kitendo cha kuanza kupata wadhamini
kama Binsulumu ambaye wamesaini mkataba misimu miwili kwa milioni 300
wamepunguza makali lakini bado fedha zinahitaji kwa ajili ya kikosi hicho hata
zile zinazotolewa na mdhamini wa ligi
hazitoshi.
Alisema kutokana na hali hiyo itakuwa vigumu kwa uongozi huo
kuendelera kutenga fedha kwa ajili ya mashabiki lakini wataendelea na utaratibu
wa awali wa kutoa vifaa vya michezo
zikiwemo jezi na vifaa vingine kwenye matawi ili fedha zinazo patikana kutokana
uuzaji vya vifaa hivyo ziweze kusadia nauali kwa mashabiki.
Hata hivyo katika hatua nyingine katibu huyo alisema kuwa ni
vema mashabiki wa timu hiyo wakashiriki kupiga vita uuzaji ya jezi feki ambazo
zinasabisha timu kukosa mapato kutokana na watu kununua jezi feki na kwamba
kila mdau wa soka ana wajibu wa kushiriki katika vita hiyo ili kunusuru wizi
huo.
‘Kwa sasa kuna jezi nyingi ni feki zinavaliwa na ndugu zenu na wangine wanaziuza
lakini tukiwa kamata na kuwa peleka polisi mna kuja mkidau ndugu zena mkiwataka
tuwafutie kesi kama kweli huyo ni ndugu
yako kwanini usaimzuie kuuza jezi feki badala ya kusubiri akamatwe ndo uanze
kusema ndugu yako?’alihoji Kimbe.
‘Ndugu zangu wapenzi na mashabiki wa soka kutoka Mkoani Mbeya ni vema mkajua wazi kuwa mnapo bariki
uuzaji wa jezi feki mitaani ndo mwanzo
wa kuuza timu hivyo ni vema tukashirikiana kwa pamoja kupiga vita uuzaji huu wa
jezi feki”.aliongeza Kimbe'
Mbali na hilo kimbe aliwaonya mashabiki wanao zomea timu za
Mkoa wa Mbeya yahani Tanzania Prisons na Mbeya na kujiita mashabiki wa Yanga na
Simba kuwa watu wamekosa uzalendo kwani hata timu hizo kubwa zinakuja mkoani
hapa kuwa vilabu hivyo vipo lakini pindi zikishuka watakosa kuona michezo wa
ligi kuu hivyo ni vema wakaungana kuziunga
timu za Mkoa wao.
Katika hafla hiyo ambayo ilishikikisha pia wachezaji wa timu
hiyo ambapo kila mmoja alikabidhiwa kitita cha sahilingi 50,000/ kutoka
wadhamini wa sherehe kampuni ya TBL kupitia kinywaji cha Castlle lager fedha
hizo zitolewa na Meneja matukio kanda ya nyanda za juu kusioni Abubakar Masohi.




No comments:
Post a Comment