Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula akifafanua
jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu
ushirikiano wa kampuni hiyo na Umoja wa Wakulima Tanzania (TASO), katika
kuhamasisha kilimo na maonyesho ya Nanenae yatakayoanza Agostii 1-8. Kulia ni Mkuu wa Biashara EAG Group, Mathew Gugai na
Mwenyekiti wa Taifa Taso, Engelbert Moyo. (Picha na Francis Dande)
Mwenyekiti wa Taifa Taso, Engelbert Moyo akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
Na Ramadhani Tembo
KATIKA
kuelekea sherehe za sikukuu ya wakulima na maonesho ya Nanenane yanayotarajiwa
kufanyika Kitaifa katika Mkoa wa Lindi kuanzia Agosti 1-8, Jumuiya
ya Wakulima Tanzania (TASO), wamejipanga kutoa mafunzo ya kilimo,uvuvi na
ufugaji bora.
Maonesho
hayo yanatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar Ally Mohamed Shein na
kufungwa na Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa (TASO), Englibert Moyo,alisema katika
sherehe hizo wakulima,wafugaji na wavuvi
watapata fursa ya kubadilishana uzoefu katika shughuli zao.
Alisema
sherehe hizo zitahamasisha jamii
kuthamini kilimo kama mkombozi wa Watanzania na tunapaswa tujifunze njia
mbalimbali za kilimo kufikia viwango vya Kimataifa.
Aidha kwa
upande wa wafanyabiashara Maonesho hayo yatatoa fursa nzuri ya kutangaza na
kupanua soko la bidhaa zao hususani pembejeo na zana mbalimbali za kilimo,
uvuvi na ufugaji nyuki.
Pia aliwaasa
wakazi wa Lindi na Mikoa ya jirani kuhudhuria katika Maonesho hayo
yanayofanyika kwa mara ya kwanza mkoani humo.
No comments:
Post a Comment