Mkurugenzi wa Amref Health Africa Tanzania Dr. Festus Ilako (wa kwanza Kushoto) Akimkaribisha Waziri wa Afya Dr. Seleman Seif Rashid kuzindua Nembo Mpya.
Waziri wa Afya, Mwenyekiti wa bodi ya kimataifa ya Amref Health Africa Mr. Omari Issa, Dr. Festus Ilako na wafanyakazi wa Amref Health Africa Tanzania katika picha ya pamoja baada ya Uzinduzi.
wadau na wageni waalikwa katika uzinduzi huo
Picha ya pamoja ya meza kuu na wadau wa Amref Health Africa baada ya Uzinduzi.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la kimataifa
lisilokuwa la kiserikali la Afrika Medical and Research Foundation (Amref) limezindua
rasmi jina na nembo yake mpya ambapo sasa litajulikana kama Amref Health Africa
Tanzania.
Uzinduzi huo
ulifanywa jijini Dar es Salaam Ijumaa ya tarehe 4/7/2014 na Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid ambapo Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa
Tanzania, Dk.
Festus Ilako, alisema
imebidi kubadili jina na nembo yao ili kuendana na majukumu yao ya sasa ambayo
yamekuwa ni zaidi ya utafiti na utoaji wa huduma za tiba.
“Kwa sasa tunajikita
pia katika uimarishaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya, mafunzo, mikakati
ya utoaji wa huduma/miradi ya afya ya mama na mtoto, ukimwi, kifua kikuu,
malaria, huduma za madaktari bingwa na maabara.
“Mabadiliko ya jina
na nembo yetu hayataathiri aina ya walengwa wetu wakuu; tutaendelea kufanya
kazi kwa karibu kabisa,” alisema Dk. Ilako.
Alitoa mfano kuwa
kila siku wanawake 22 wanapoteza maisha nchini wakati wa kujifungua na kwamba
mpango wa Amref ni kupunguza vifo hivyo.
Waziri Seif katika
hotuba yake ya uzinduzi, alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa taasisi
hiyo na kwamba wamesaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU)
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, mimba za utotoni na upatikanaji wa majisafi
na salama.
No comments:
Post a Comment