Katibu Mkuu wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Dk. Willibrod Slaa akifafanua jambo katika sikukuu ya wahisani ya umoja wa
wanafunzi wa kikatoliki (TYCS) iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto
ni Mlezi wa umoja wa wanafunzi hao, Dustan Haule na Mwenyekiti, Johnson Kaaya.
(Picha na Francis Dande)
Na Mwandishi Wetu
KATIBU
Mkuu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
D.k Willibrod Slaa ameitaka serikali kubadilisha mfumo mbovu wa elimu uliyopo
sasa ili kuweza kuchenga taifa la wamisomi wailiyoelimika si bora wasomi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,
katika sikukuu ya wahisani ya umoja wa wanafunzi wa kikatoliki (TYCS), alisema
kuwa msingi mmbovu wa elimu uliyopo ndiyo chanzo cha kuzalisha wasomi
waliowengi lakini hawana sifa katika soko la Dunia.
“Mimi nashangaa kuona nchi hii,
inabadilisha mfumo wa zamani ambao ulikuwa ukimfanya mwanafunzi kujisomea kwa
bidii na kupata wasomi walio na maarifa na uchungu na nchi yao, lakini hivi
sasa mwanafunzi analetewa mtihani wa kuchagua majibu, huu ni uzembe kwa mamlaka
husika,” alisema.
Aliongezea kuwa, wazazi nao wanapaswa
kuwafuatatilia watoto wao kwa ukaribu mkubwa katika masomo na maisha yao kwa
ujumla, ili kuweza kutambua mapungufu ya mtoto na kuweza kuyatafutia ufumbuzi
mapema.
Pia aliwataka wazazi, kuwapa fursa watoto
endapo amengundua kuwa anakipaji na kuweza kukiendeleza kuliko kuona na
kupuuzia jambo ambalo anauwa ndoto zao.
D.k Slaa, aliwataka vijana wote hususani
wanafunzi, kutokujihusisha katika mambo mabaya yasiyompendeza mwenyezi Mungu
yakiwemo Ulevi, Uzinzi, matumizi ya Madawa ya kulevya, rushwa na kuiga mambo
ambayo hayana manufaa kwao ili kuweza kutimiza ndoto walizonazo kwa manufaa ya
kwao na taifa kwa ujumla.
Naye Katibu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam
TYCS, Yohana Deogratias alisema kuwa madhumuni ya umoja huo ni kuwasaidia
wanafunzi kutambua haki na wajibu wao na kuweza kumjenga mwanafunzi kiroho.
Aliongezea kuwa, jimbo hilo lina jumla ya
kanda 16 na matawi 250, pia aliwataka wakuu wa shule na walezi kuweza
kuwaruhusu wanafunzi kuweza kushiriki matukio mbalimbali ya chama hicho ili
kuweza kuwajenga kiroho.
No comments:
Post a Comment