WATANZANIA wametakiwa
kuwaadabisha kwa kutowachagua viongozi mafisadi wanaotaka kuingia madarakani
kwa kutumia fedha chafu, katika chaguzi zijazo.
Kauli hiyo, ilitolewa na
Mwenyekiti wa Bodi ya Madini nchini, Richard Kasesela wakati wa ibada ya
kuiombea nchi amani na mafanikio ya ujenzi wa Chuo cha Biblia mkoani Mbeya, yalifanyika
katika Kanisa la Hossana Life Mission jijini Dar es Salaam.
Alisema endapo mafisadi hao
wataingia madarakani katika cha guzi za Serikali za Mitaa zinazotarajiwa
kufanyika hivi karibuni na uchaguzi mkuu mwakani, kuna hatari amani ya nchi
ikatoweka.
Kasesera, alisema kiongozi
yeyote anayeweka fedha mbele hawezi kusimamia utawala wa sheria ambao unaweza
kusimamia utekelezaji wa haki, kitendo ambacho kitawasukuma wananchi kutafuta haki yao kwa kutumia nguvu.
“Nchi inakabiliwa na
viashiria vya uvunjivu wa amani kwa watu kunuka damu kwa mfano wapo watu
wanawaua vikongwe bila hofu kwa imani za kishirikina hii ni ishara mbaya, nchi
iliyozoeleka kuwa ya yamani na utulivu kumbe huku nyuma kuna kazi,”alisema
Kasesera.
Alisema, jukumu la kulinda
amani ni la wananchi wenyewe, na hiyo itawezekana pale watakapoamua kuchagua
viongozi bora na wala sio mafisadi, akibainisha kuwa wanawajua wanaofaa na
wasiofaa kwani watu hao wanaishi nao huko mitaani.
Akizungumzia Ujenzi wa Chuo
hicho, Kasesela, alisema madhui yake ni mazuri ambapo pia alishauri
kitakapokamilika kianzishe mafunzo ya upatanishi wa viongozi wa Afrika, kwani
baadhi ya nchi viongozi wake wamejikuta katika migogoro ya kugombea madaraka na
matokeo yake ni kuvuruguka kwa amani.
Kasesela japo fedha
zinazohitajika katika ujenzi wa chuo hicho ni nyingi hata hivyo anaamini
zitapatikana.
Awali, Askofu wa Kanisa hilo,
Ephraim Mwansasu, alisema chuo hicho kitakapokamilika kitakuwa cha kwanza katia
chi za Afrika zilizoko chini ya Jangwa la Sahara kwa kutoa mafunzo ya utambuzi
wa Gharama ya Amani inapotoweka katika nchi husika.
Alisema wamefikia uwamuzi
wakuwa na mafunzo hayo kwa sababu hivi sasa viongozi mbali wa dini na siasa
wamekuwa wakiizungumzia uwepo wa amani lakini bila kutoa ufafanuzi kuhusu
gharama zake katika maisha ya wananchi.
Katika rambee iliyofanyika
Septemba saba mwaka huu jijini Dar es Salaam, Kanisa hilo lilikusanya sh
milioni 100 wakati harambee hiyo ikiwa bado inaendelea katika makanisa mengine
yaliyoko ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment