Na Mwandishi Wetu
KOCHA maarufu nchini na nyota wa zamani wa Klabu ya
Simba, Majimaaji na timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Abdallah ‘King Mputa’
Kibaden, ameibuka na kusema hajafa na kwamba yu mzima wa afya.
Kibadeni aliyasema hayo baada ya kutafutwa kwa njia ya simu kupata uhakika kama yu hai kweli, kwani baadhi ya mitandao ya
kijamii ilikuwa imeripoti kuwa nguli huyo wa soka nchini amefariki.
Baada ya kupokea simu, Kibaden alitoa pole kwa wote
waliopata taarifa za kifo chake na kushtuka kwani yeye yu umzima wa afya.
Kibaden alionyeshwa kushangazwa na kitendo hicho cha
kuzushiwa kifo akisema ni dalili za baadhi ya watu kumtakia mabaya.
Alisema kutokana na taarifa hizo za kifo feki kisambaa
kama moto wa nyika, kwa kutwa ya jana alipata usumbufgu mkubwa wa kupokea simu
kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wanaomfahamu.
"Mimi nipo
nyumbani nikiwa mzima wa afya. Nashangazwa na habari kuwa nimefariki dunia. Nina
wapa pole wale wote waliopata mshtuko kwa ajili yangu.
“Kuna wengine wananipigia, wakisikia sauti yangu,
wanapatwa na mshituko... wapo waliomwaga machozi," alisema Kibaden kwa
utulivu.
Kibadeni alisema, siku ya jana haikuwa usumbufu mkubwa
kwake tu, bali hata kwa familia yake ambayo ilipokea simu nyingi za watu
wakiwapa pole juu ya kifo changu.
Hata hivyo, Kibadeni alishukuru kwa baadhi ya vyombo vya
habari vilivyomtafuta kwa simu kupata uhakika akimini vitasaidia kufikisha
ujumbe kwamba ni uzushi.
“Ni vizuri mlivyonipigia simu, naamini mmetaka kupata
ukweli wa taarifa hizo mbaya dhidi yangu. Mimi ni mzima wa afya,” alisema na
kuongeza:
"Kutwa ya leo (jana) mimi na familia yangu tumepata
mshtuko mkubwa. Jamani si kweli, mimi ni mzima wa afya niwape pole wote
waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizi za uzushi. Sijui mtu kazipata wapi?
Aidha, Kibaden alisema pamoja na kwamba hakuna mwanadamu
atakayeishi milele, lakini anamshukuru Mungu bado yu hai hadi pale muumba wake
atakapoamua.
Tanzania Daima
ilipowasiliana na mtandao wa Taarifa.com,
simu yao ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
Hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) imekuwa ikionya juu ya mitandao ya kijamii kuandika ama kutoa taarifa
ambazo si sahihi.




No comments:
Post a Comment