HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 07, 2014

MEMBE azindua mfuko wa elimu UB

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) akipokelewa na Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo wakati wa mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Kiromo Bagamoyo Mkoa wa Pwani. (Picha na Francis Dande)
 Mkuu wa Kitivo Cha Sheria Cha Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana kwa bashasha na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. 
 Mgeni rasmi akisalimiana na Jaji Steven Mbwana.
Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Sheria.
 Bendi ikiongoza maandamano.
 WahitimuM
 Mgeni rasmi akiingia kwa maandamano.
 Baadhi ya wahitimu.
 Wahitimu
Wahitimu.
Wajumbe wa Bodi
 Wajumbe wa Bodi
 Ofisa Habari wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Happiness Katabazi (kushoto) akiwa katika mahafali hayo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe akifungua rasmi shughuli za mahafali hayo.
Baadhi ya waadhili wa Chuo kikuu cha Bagamoyo.
  Mkuu wa Kitivo Cha Sheria Cha Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto)
 Mgeni rasmi (kushoto) akifurahia jambo na Makamu Mkuu wa ChuoKikuu cha Bagamoyo, Prof. Costa Mahalu.
 Wazazi wakiwa katika mahafali hayo.
 Wageni mbalimbali wakifuatilia mahafali hayo.
 Wahitimu.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Prof. Costa Mahalu akizungumza wakati wa mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Kiromo, Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Dk. Williamu Kudoja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushhirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiwatunuku Shahada mbalimbali wahitimu.
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza katika mahafali hayo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza katika mahafali hayo.
Ofisa Habari wa UB, Happiness Katabazi akikabidhi zawadi ya mgeni rasmi.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Prof. Costa Mahalu akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akishirikiana na Prof. Mahalu kukata keki.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akimlisha keki mtangazaji wa TBC1 Shaaban Kisu.
 Mgeni rasmi akilishwa keki.
 Makamu Mkuu wa Chuo akilishwa keki.
 Jaji Steven Mbwana akitoa neno la shukrani.
  Picha ya pamoja.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chuo.

Na Happiness Katabazi, Pwani

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe amezindua mfuko wake wa elimu Katika Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), ' utakaojulikana kwa jina la ' Bernad Membe Scholarship 'Membe kwaajili ya kusaidia vijana wenye maitaji Maalum.


Membe aliyasema hayo Juzi Katika Viwanja Vya Hoteli ya Kiromo , iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani katika sherehe za Mahafali ya pili ya UB  na Kisha aliwatunuku jumla ya wahitimu 90 Shahada ya Uzamili,shahada ya kwanza, Diploma na Cheti wahitimu wote hao.

 
Membe ambaye alikuwa ni mgeni rasmi amefikia uamuzi huo wa yeye binafsi kaunzisha  mfuko wake huo wa elimu ndani ya UB, kwasababu yeye anaamini kuwa elimu ni Taa na ufunguo wa maisha ya binadamu yoyote hasa katika ulimwengu huu wa sayansi na kwamba kuna vijana wanaitaji kupata elimu ya juu lakini wazazi wao hawana huwezo wa kuwalipia Ada.


"Binafsi naamini ukimlipia kijana Ada ya chuo utakuwa umempatia kitu kikubwa sana kijana. ...hivyo mfuko wangu huu wa elimu niliyouanzisha hapa UB ,utasaidia Makundi hayo maalumu kulipiwa Ada ya chuo ...na nitayari nimeishaanza kufanya mazungumzo na baadhi ya watu wenye Fedha ili waweze kuingiza Fedha Katika mfuko huo  na ninawaomba matajiri ambao Mungu amewajilia kuwa na uwezo kiuchumi waanze kuchangia Fedha Katika elimu ili vijana wetu kote nchini ambao hawana uwezo wa kulipa Ada Fedha hizo zilizotolewa matajiri ziweze kuwasomesha "  alisema  Membe na kushangilia.


Kwa  upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Professa Costa Mahalu alisema anamshukuru Membe kwa uamuzi wake kimaendeleo kwa kuanzisha Mfuko huo , UB kwasababu hata sera ya bodi ya mikopo bado haitosholezi Mahitaji ya wahitaji wa mikopo ya kusoma elimu ya juu.


Profesa Mahalu alisema Taifa linaitaji kuongeza jitihada za Kuzalisha wahitimu bora wa elimu ya juu ili wasomi hao wawewe kuingia kwenye mapambano ya kuwatokomeza maadui watatu ambao ni ujinga,maradhi na umasiki na pia waweze kwenda kushindana katika soko la ajira katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

 
Aidha Profesa Mahalu alisema kuanzia Januari mwakani, UB itaanza kujenga makazi yake ya kudumu katika kijiji cha Kiromo Bagamoyo  ambapo ujenzi ukikamilika kutakuwa NA uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 5000.

No comments:

Post a Comment

Pages