NA
MWANDISHI WETU, TANGA
TIMU
ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya”imeanza maandalizi kabambe kujiandaa na mechi
yake ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi yao na Polisi Morogoro itakayo
chezwa Jumamosi wiki.
Mechi
hiyo inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni muendelezo wa
Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara iliyoanza kutumia vumbi Septemba 26
mwaka jana.
Akizungumza
leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa baada ya kumalizika
mechi yao na JKT Ruvu,Kocha Mkuu wa timu hiyo,Mkenya James Nandwa akishirikiana
na Mkurugenzi wa benchi la Ufundi Mohamed Kampira na Kocha wa Makipa Mfaume
Athumani walikwisha kuyafanyia kazi mapungufu yaliyopelekea kupoteza mchezo
huo.
Assenga
amesema kuwa sasa baada ya kazi kubwa iliyofanywa na makocha hao kikosi hicho
kipo kamili kuweza kuwavaa maafande wa Jeshi la Polisi kutoka mkoani Morogoro
ili kuweza kuhakikisha wanabakiza pointi tatu muhimu .
Amesema
kuwa licha ya kuhakikisha wanapata matokeo mazuri lakini wachezaji wanaounda kikosi hicho wamepania kuonyesha
kandanda safi ili kuweza kuwapa burudani wapenzi na mashabiki wa soka mkoani
hapa.
Coastal
Union iliyopo nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara imepania kufanya vizuri katika michezo yake iliyosalia kwenye mzunguko wa
kwanza ili kuweza kupaa kileleni mwa ligi hiyo.
Mwisho.
IMETOLEWA
na Kitengo cha Mawasiliano Coastal Union.
Ofisa
Habari wa Coastal Union.
Oscar
Assenga.
0714543839




No comments:
Post a Comment