Mfungaji wa timu ya Temeke, Fatuma Mchenga akimiliki mpira katikati ya
wachezaji wa timu ya Dodoma, katika
mashindano ya Taifa ya Netiboli kwenye Uwanja wa Sigara Chang'ombe jijini Dar
es Salaam. Temeke ilishinda 24-21.
Mshambulia wa timu ya Temeke, Matalena Mhagama (kushoto) akimiliki mpira
huku akizongwa na mchezaji wa timu ya Dodoma, Magreth Matiko wakati wa michuano
ya Netiboli ya Taifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Sigara Chang’ombe jijini
Dar es Salaam. Temeke ilishinda 24-21.
Mchezaji wa kati wa timu ya Temeke, Betina Kazinja (katikati) akimiliki mpira huku akizongwa na wachezaji wa timu ya mkoa wa Dodoma wakati wa michuano ya Netiboli ya Taifa.
Mshambuliaji wa pembeni wa timu ya Temeke, Faraja Malaki (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka Mwamvita Mohamed katika michuano ya Netiboli ya Taifa.
Kikosi cha timu ya Temeke.
Kikosi cha timu ya Mkoa wa Dodoma.
Wachezaji wa timu ya Temeke.




No comments:
Post a Comment