HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

January 09, 2015

Mkubwa Fella apania kurejesha soko la albam

Mkubwa Fella
MKURUGENZI wa taasisi ya muziki wa Bongo ya Mkubwa na Wanawe, Said Fella 'Mkubwa Fella' amesema kuwa, kwa kutumia ukongwe wake katika tasnia hiyo, atahakikisha anarudisha soko la albamu kama ilivyokuwa zamani.

Kwa mujibu wa Mkubwa Fella, licha ya wasanii wengi kukataa kutoa albamu wakihofia soko lake kuporomoka, atahakikisha albamu ya Yamoto Band itauza na kurudisha faida.

Alisema kuwa, yeye ndio meneja wa kwanza wa muziki huo hapa nchini, hivyo kwa kutumia ukongwe huo atatumia akili za ziada ili kugundua tatizo lilipo na kujitahidi afanye kile anachokusudia.

"Mtu mzima ni mtu mzima tu, mimi nitahakikisha narehesha soko la albamu, unajua msanii anajiona bora pale anapokuwa na albamu na hawa wasanii wa Yamoto ni wadogo hivyo natakiwa kuwakuza kimuziki unaotakiwa, mimi nitalazimisha kuwashawishi hao wadau mpaka soko litarudi," alisema.

Wasanii walio wengi kwasasa wamesitisha utoaji wa albamu kutokana na kutokuwepo kwa soko hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages