Wanafunzi wa Madrasa Shathil ya Chang’ombe jijini Dar es
Salaam wakisoma Qaswida wakati wa sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad
(S.A.W.) zilizofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama
Zakia Bilali (katikati) akiwa na Wake wa makamo wa Pili wa rais wa
Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (kushoto) na Mama Pili balozi Seif
(kulia) pamoja na Wake wa Viongozi mbali mbali na wananchi wa kawaida
wakijumuika katika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume
Muhmmad S.A.W
yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja
ambapo hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita. (Picha na
Ikulu, Zanzibar)
Ustadh salum Rashid kutoka Amani Wilaya ya Mjini Unguja
akisoma Mlango wa Barzanji(4) wakati wa sherehe za Maulid Matukufu ya
kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.)
zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele
ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein.
Akina Mama kutoka mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja na
Vitongoji vyake wakiwa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja
palipofanyika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad
S.A.W ambapo hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita na
mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj
Dk. Ali Mohamed Shein na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi
(katikati) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Kadhi Mkuu wa
zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) Waziri wa katiba na Sheria Abubakar
Khamis Bakary akifuataiwa na makamo wa Pili wa Rais Alhaj Seif Ali Iddi
wakisimaa kwa pamoja na waislamu wengine na Viongozi wakati wa Kumswalia
Bwana Mtume Muhammad S.A.W.katika sherehe ya Maulid iliyofanyika jana
viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja.
Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa katika maandamano ya sherehe
za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Wanafunzi wa Madrasatul Dhuriyatul Islamia kutoka Kisiwani
Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja wakisoma Qaswida wakati wa sherehe za Maulid
ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika katika viwanja vya Maisra
Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein. (Picha na Ikulu, Zanzibar)







No comments:
Post a Comment