HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 23, 2015

AISHI NA KINYESI NDANI YA CHUMBA CHAKE KWA MIAKA 2

Kinyesi kilichokutwa chumbani.
Na Mwandishi Wetu

MWALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Abert ameishi na kinyesi, mikojo, mende na funza wa kila aina katika chumba kimoja kwa muda wa miaka miwili.

Tukio hilo ambalo limewafanya majirani kujiuliza maswali ambayo wamesema hawajayaptia majibu, limetokea juzi jioni, Mtaa Yombo Kisiwani wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.

Reuben Shayo, ambaye ni miliki wa nyumba hiyo, alisema Gaudensia alikuwa mpangaji wake, hakuwa mkorofi alikuwa akilipa kodi bila matatizo.

Alisema, uchafu huo uligundulika baada ya chumba hicho kufuka wingu la moshi uliyowafanya wapangaji wenzake kudhani kinataka kuwaka moto hali iliyowafanya wa mwite yeye ili washuhudie kilichokuwa kikiendelea.

“Tulikisogelea chumba chake nikamwiita na kumuuliza kuna nini mbona kuna wingu la moshi akajibu hakuna kitu, nikamtaka afungue akagoma ndipo nikamtisha kumuitia polisi endapo angeendelea na msimamo wake huo wakukataa kufungua,”alisema Shayo.

Alisema baada ya kusikia hivyo, alikubali  kufungua mlango, hata hivyo kile walichotegemea kukiona hawakiona na baadala yake waligundua hali hiyo ya uchafu ambao wanashindwa kuuelezea kwani haukuwa wa kawaida ambao mwanadamu asingeweza kuishi nao.

Shayo, alisema uchafu huo wa kinyesi, mikojo na majimaji mengine machafu ulihifadhiwa katika vyombo mbalimbali ikiwemo ndoo, masufuria, visadolin, ndoo za plasti, chupa, magudulia.

“Kuna vinyeshi yani sio uchafu kama makaratasi ni maji yenye utandu, yaliyovunda yakichanganyika na funza na mende waliosambaa chini na juu ya vyumba vyake hivyo viwili ambako anapikia humo, sielewi lengo lake lilikuwa nini,”alisema Shayo.

Shayo, alisema harufu na mazingira ya vyumba hivyo sio ya kumfanya mtu yeyote aishi katika mazingira hayo ukichukulia kuwa huyu ni msomi, tena mwalimu wa sayansi.

Aidha, alisema mwalimu huyo, ni mtu wakujitenga na wezake kwa mfano hutamuona nje akikaa na wenzake siku anapoonekana ni wakati wa zamu yake ya kufanya usafi.

Aliongeza kuwa mwalimu huyo hana rafiki wala haijatokea hata siku moja akatembelewa na mtu pia haruhusu hata wapangaji wenzake kuingia chumbani.

“Hali hii inatutia mashaka inafikia pahala hata tukimuona mtu amesoma tushindwe kumuamini,”alisema Shayo.

Reuben, alisema mwalimu huyo hastahili kuishi na jamii, kutokana na mazingira hayo anatakiwa ajenge nyumba yake kisha aishi pekee yake.

“Tumejiuliza sana tukadhani labda alikuwa anafanya utafiti lakini haiwezekani kwa wingi wa uchafu ule, kama ingekuwa ni utafiti angehifadhi japo katika kichupa kimoja,”alisema.

Shayo, alisema kwa vile hadi jana alikuwa plisi ambako alipelekwa kwa ajili ya usalama wake, atakaporudi itabidi ahame lakini lazima afanye usafi ambao ataomba usimamiwe na maofia wa afya ili kuepusha madhara.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Yahya Bwanga, alikiri, kushuhudia tukio hilo, na kusema kwa maisha ya binadamu wa kawaida tena mwenye sifa kuwa mwalimu anayetegemewa na taifa kuishi katika mazingira kama hayo imempa shida hadi ashindwe kuelewa.

Aliwataka polisi kulipa suala hilo uzito ili jamii iweze kufahamishwa kilichokuwa kikiendelea kwa vile tukio hilo liko wazi sasa hakuna haja ya kulindana.

“Hili jambo sio dogo, wengine walikuwa wakitaka apewe notisi ahame tu jambo ambalo halikubaliki, mwalimu anaaminika halafu leo anakuja kujihusisha na vitendo vinavyoleta mashaka ya kishirikina katika jamii,”alisema Bwanga.

Bwanga, aliongeza kuwa atawasiliana na Mtendaji wa Kata ili waweze kulishughulikia kwa pamoja wakati mwalimu huyo akiwepo.

No comments:

Post a Comment

Pages