NA
BRYCESON MATHIAS, MOROGORO
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tawi la Mbigili wilayani Kilosa, kimesema
kitamng’oa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho wa Chama cha Mapinduzi (CCM),
Hemed Ibrahim Salim, kama ataendelea kutoitisha vikao kwa kisingizio cha
kuogopa kukataliwa kwa kukosa taarifa ya makabidhiano.
Akizungumza
mtandao huu, Mwenyekiti wa Chadema wa tawi hilo, Maftaha Hamis,
alimtuhuhu mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho kwamba alichapisha vitabu vya
risiti za michango kwa ajili ya ufuatiliaji wa mgogoro wa wakulima na wafugaji,
ikidaiwa fedha hizo zilizokusanywa zimetafunwa.
Awali
ilifahamika kwamba, Mwenyekiti Salum anabanwa kuhusu taarifa ya makabidhiano ya
serikali ya Kijiji hicho kwa sababu, kabla ya kuchaguliwa Desemba 14, mwaka
jana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa kuwa alikuwa mwenyekiti wa mpito,
baada ya aliyekuwa mwenyekiti kujiuzulu.
Hamisi
alisema: “Kuna risiti feki alizochapisha na kugonga mhuri wa halmashauri
kisiri, ambapo wakulima waliopo kijijini cha mbigili, walichangishwa sh. 2,000
na wakulima wa Mbigili wanaoishi Morogoro mjini walichangia sh. 5,000, lakini
kwa masikitiko, fedha hizo zilitafunwa.”
Mbali
ya fedha zenye risiti feki kutafunwa, Mwenyekiti Hamis wa Chadema alidai sababu
nyingine za kumng’oa Mwenyekiti wa CCM, Salim, ni pamoja na sintofahamu ya
ziliko fedha za ruzuku ya kijiji sh. milioni 15 na mifuko ya saruji 50 za Mfuko
wa Maendeleo wa Rais (TASAF), ambazo hazijulikani ziliko.
Aidha
Hamis aliongeza kutoa madai kwamba, bado kuna sintofahamu kuhusu Shule ya
Sekondari ya Mazoezi ya Mbigili, ambayo imekuwa haifahamiki kama imesajiliwa au
la, kwa sababu tayari imetumia fedha nyingi kuikarabati na wananchi wamechangia
nguvu zao kwa kiwango kikubwa.
Awali
Mwenyekiti Salim alipohojiwa dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, alikanusha
vikali na kudai kuhusu mifuko 50 ya saruji, anatakiwa ahojiwe aliyekuwa
mwenyekiti kabla yake, ili kujua waliitumiaje na aliyekuwa mkandarasi wa
Sekondari ya Magore, na kuhusu sh. mil. 15, alisema zilipopelekwa kijijini hapo
zilipokewa zikiwa na maagizo ya uongozi wa Wilaya ya Kilosa ya nini zifanyike.
No comments:
Post a Comment