Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Uwekezaji na
Uwezeshaji) Mhandisi Christopher Chiza (Mb) akibadilishana mawasiliano na
baadhi ya wafanyabiashara waliowasili Visiwa vya Comoro kwa ajili ya kushiriki
katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro,
linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 Aprili, 2015. Kushoto ni
Balozi wa Tanzania Visiwa vya Comoro, Chabaka Kilumanga.
Waziri
wa NChi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhandisi
Christopher Chiza akiwa na wenyeweji
wake baada ya kuwasili visiwani vya Comoro. Kushoto ni Balozi
wa Tanzania Nchini Comoro, Chabaka Kilumanga.
Na Mwandishi Wetu, Comoro
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (Mb)
ahudhuria Kongamano Kubwa la Biashara kati ya Comoro na Tanzania,
litakalofanyika tarehe 23 Aprili, 2015 Visiwani Comoro.
Lengo kuu la kongamano hilo
ni “kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro kwa
kutambua fursa zilizopo kati ya nchi hizi mbili na kurasimisha biashara ambayo
kwa sasa hairatibiwi”.
Kongamano
hilo ambalo litawakutanisha viongozi, maafisa wandamizi wenye dhamana ya
kuendeleza biashara kutoka Tanzania na Comoro pamoja na wadau wa Sekta Binafsi, litafungua rasmi fursa
ya kutangaza na kuuza bidhaa zinazozalishwa Tanzania kwa wafanyabiashara
watakaopenda kufanya hivyo kutokana na nafasi nyingi za biashara na uwekezaji
zilizopo katika Visiwa vya Comoro.
Miongoni
mwa mada ambazo zitazungumzwa katika kongamano hilo ni pamoja na; Mada kadhaa kuhusu fursa za biashara na uwekezaji
nchini Tanzania na Comoro, mazingira ya biashara za uwekezaji nchini Tanzania
na Comoro, fursa zinazopatikana katika nchi hizo na usaidizi wa kiserikali
katika kurahisisha baishara. Aidha, itakuwapo fursa ya mazungumzo ya kina kati
ya wafanyabiasha wa Comoro na Tanzania (business to business discussions).
Aidha,
zipo fursa nyingi za uwekezaji katika uzalishaji na usindikaji wa bidhaa za
kilimo, pamoja uwekezaji katika sekta ya huduma za afya, elimu, mawasiliano na nishati
endapo fursa hizi zitatangazwa na kuwekwa miundombinu ya uhakika ya usafiri
kati ya Tanzania na Comoro bidhaa za Tanzania zitapata soko la uhakika visiwani
Comoro.
Kongamano
hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na wafanyabiashara na wadau mbalimbali kutoka Tanzania, limeandaliwa na Ubalozi wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania nchini Comoro, kwa kushirikiana na kampuni ya
361 degrees ya Dar es Salaam.
Kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali, ikiwa ni
pamoja na Mamlaka ya Uendelezaji wa Biashara Tanzania (TANTRADE) ambao
wanahamasisha na kuwakaribisha wafanyabiashara wa Tanzania, Exim Bank, Shirika
la Ndege la Air Tanzania, Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima
ya Comoro (UCCIA); na Mamlaka ya Kuendeleza Vitega uchumi vya Comoro (INM).
No comments:
Post a Comment