HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 17, 2015

RAZA AWAPONDA WANAOTUMIA FEDHA KUWANIA MADARAKA

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohammed Raza, ameshtushwa na baadhi ya wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano kumwaga mabilioni yafedha chafu Zanzibar ili kuwashawishi baadhi Wajumbe wa chama hicho kuwaunga mkuno katika mbio hizo.

Tanzania hivi sasa iko katika harakati za Uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwakufanyika Oktoba mwaka huu.

Raza ambaye ni Mwakilishi wa Uzini, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati alipozungumza na wandishi wa habari, kuhsu mustakakabali wa kupatikana Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa vile hilo ni suala nyeti katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
“Suala hili lina unyeti wake kwani linagusa hadi majeshi na mahakama amabao nao wanapaswa kujua sifa za rais ajaye, hivyo haitakuwa busara kwa rais wa nchi apatikane kwa njia ya rushwa.

Alisema hivyo kwa vile kuna baadhi ya wawagombea wanafasi hiyo, wakishirikiana na wafanyabiashara tayari wanaendelea na mchezo huo mchafu wa kutoa rushwa waziwazi huku hata Kamati Kuu ya Chama Ikishindwa kukemea vitendo hivyo vya hatari kwa nchi.

“Nazungumzia chama changu, tumeingia kwenye uchaguzi mkuu, naamini bado tunakazi ya kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi hatujamaliza kazi, sasa kama sisi viongozi tunaona mabilioni ya rushwa yakiingizwa dhahiri bila ya kukemewa imenishtua,”alisema.

Raza, alisema kitendo cha kupatikana rasi iliyetokana na misingi ya rushwa, itafika wakati rais huyo atashindwa kuwa na maamuzi ya kuongoza nchi na baadala yake atakuwa akitekeleza matakwa ya magenge ya watoa rushwa.

“Tunapompata rais ambaye amechaguliwa kwa misingi ya rushwa Watanzania wajue kuwa atakuwa akielezwa na waliomuingiza madarakani kwamba mchague huyu au yele ashike wizara fulani kwa ajili ya maslahi yao, lakini pia chama changu lazima kijue kuwa kuna Ukawa na CUF ambao nao wanataka kuingia madarakani,”alisema Raza.

Akizungumzia Suala Akaunti ya Tegeta Escrow, Raza, alisema kuwa Wazanzibar wanamtaka Waziri wa Fedha, atoe tamko atalifidiaje pengo Zanzibar kukosa misaada kutokuna naTanzania kuwekewa vikwazao na wahisani kutokana na kashfa ya Akaunt ya Tegeta Escrown.
Alisema, hivyo kwa vile kashfa hiyo haiwahusu  Wazanzibari, kwani halikuwa suala la muungano bali lilikuwa la Bara.

Hata hivyo, Raza, alisema bado viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibarr, wanatakiwa kuacha woga na baadala yake wajenge hoja kwa kuwaambia wahisani kuwa suala hilo haliwahusu Wazanzibari.
“Mwaka 1995  Zanzibar, iliwekewa vikwazo na huku bara ikidai kuwa iliambiwa na wahisani isiwape misaada, lakini kwa hili la Escro, viongozi wa Zanzibar walitakiwa kujenga hoja kwamba haliwahusu, angalia pale hakukua hata na Mzanzibari aliyehusika katika kashfa ya Tegeta Escro,”alisema Raza.
Raza, alisisitiza kuwa hata wakati wa EPA wazanzibari hawakuhusika lakini waliingizwa akibainisha kuwa hayo yote yanatokea kutokana na woga wa viongozi wa Serikali ya Zanzibar.
Aidha, Raza amesistiza kuwa alifuatilia suala hilo la vikwazo ili ikiwezekana Zanzibar iweze kuondolewa vikwazo hivyo ambavyo anaamini haviihusu Zanzibara.
 Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi jimbo la Uzini (CCM), Mohamed Raza ( kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya mustakabali wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Vincent Tiganya. PICHA: MPIGAPICHA WETU

No comments:

Post a Comment

Pages