SHIRIKA
LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwapo tatizo la
upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu
chini ya jiji la Dar es salaam, pamoja na baadhi ya maeneo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na
mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 48 kuanzia siku ya Jumamosi 23/01/2016
hadi Jumapili 24/01/2016.
Taarifa
ya kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na kaimu meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi Everlasting Lyaro, imeeleza kuwa sababu ya
kuzimwa kwa mtambo huo, ni kuruhusu mkandarasi kuunganisha bomba jipya na bomba
la zamani katika tanki la Maji wazo-Tegeta, zoezi ambalo linaashiria kukamilika
kwa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini, hivyo kuondoa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika
maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini.
“Tunaelekea
kwenye hatua za mwisho za kupokea Maji mengi kutoka mtambo wa Ruvu Chini baada
ya kazi ya upanuzi inayoelekea kukamilika mapema mwezi February mwaka huu, na
kiasi cha Maji kitaongezeka kutoka wastani wa Lita Milioni 182,000
zinazozalishwa sasa hadi Lita Milioni 270,000. Hivyo kuzimwa kwa mtambo huu ni
moja ya hatua za mwisho-mwisho katika ukamilishaji wa Mradi wa Ruvu Chini”
alisema Lyaro
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, DAWASCO imetoa wito kwa wateja na wananchi wote
kuhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi muhimu ili kukidhi mahitaji
husika kwa kipindi hicho chote.
Taarifa
hiyo imeeleza kuwa matengenezo hayo yatasababisha maeneo mengi ya jiji la Dar
es salaam kukosa Maji, pamoja na mji wa Bagamoyo vijiji vya Zinga, Kerege na
Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe.
Maeneo
mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Kijitonyama,
Kinondoni, Oysterbay, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Muhimbili,
Buguruni, Chang’ombe na Keko
No comments:
Post a Comment