Mnamo tarehe 15 Januari 2016 Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa taarifa kwa umma kuhusu kufungia Watoa
Huduma za Maudhui ya Utangazaji (Redio na Televisheni) 27 waliokuwa wanadaiwa
ada na tozo mbalimbali zinazotokana na leseni zao. Aidha,tarehe 18 Januari 2016
ilichapichwa taarifa ya makampuni ambayo yatafungiwa kwa muda ikiwa watashindwa
kulipa ada na tozo hizo katika magazeti mbalimbali. Nia ilikuwa kuwakumbusha
kwa mara ya mwisho utekelezaji wa wajibu wao kwa mujibu wa sheria na masharti
ya leseni.
Baada ya taarifa hizo katika magazeti
Mamlaka ilipokea maombi kutoka katika vituo vingi vikiomba kutokufungiwa vituo
vyao na kwamba waruhusiwe kufanya malipo siku hiyo ya tarehe 18 Januari 2016 na
kuwasilisha stakabadhi katika ofisi za TCRA kuthibitisha kuwa malipo
yamekamilika. Mamlaka ilikubali maombi hayo na hadi kufikia mwisho wa saa za
kazi tarehe 18 Januari 2016, redio 12 kati ya 20 na kituo kimoja kati ya vituo
vya television 6 vimelipa ada na tozo zote au kubakiza kiasi kidogo cha deni
ambalo walikuwa wanadaiwa na hivyo kuviruhusu kuendelea kutoa huduma ya
utangazaji kama kawaida. Kwa wale ambo hawajamaliza malipo yote Mamlaka
inaingia nao mkataba maalumu wa lini bakaa la deni litalipwa, na kwamba
wasipofanya hivyo kwa muda uliokubalika hatua nyingine za kisheria
zitachukuliwa.
Hadi kufikia tarehe 19 Januari 2016
ni vituo 13 ambavyo havijaweza kulipa deni wanalodaiwa na wala hawajawasiliana
na Mamlaka. Hivyo basi Mamlaka imeendelea na utekelezaji wa sheria wa kusitisha
utoaji wa huduma za utangazaji kwa vituo vya redio na television vilivyoorozeshwa
hapa chini, hadi hapo watakapotekeleza wajibu wao wa kulipa ada na tozo
wanazodaiwa. Hii inamaanisha ya kuwa vituo hivi vitafunguliwa pindi
watakapolipa ada na tozo husika. Ikiwa watashindwa kufanya hivyo kwa muda wa miezi
mitatu kuanzia tarehe 19 Januari 2016 hatua zaidi za kisheria kwa mujibu wa Kifungu
22(a) cha Sheria ya EPOCA ya Mwaka 2010 zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja
na kufuta leseni zao za kutoa huduma ya utangazaji.
Vituo vilivyofungiwa ni;
1. Breeze FM ya Tanga
2. Country FM Radio ya Iringa
3. Generation FM Radio ya Mbeya
4. Hot FM Radio ya Mbeya
5. Impact FM ya Dodoma
6. Kifimbo FM Radio ya Dodoma
7. Rock FM Radio ya Mbeya
8. Iringa Municipal
TV
9. Sumbawanga
Municipal TV
10. Tanga City TV
11. Mbeya City
Municipal TV
Mamlaka inapenda kuwakumbusha makampuni
yote yaliyopewa leseni ya kutoa huduma za utangazaji wa redio na televisheni na
huduma zingine zote zinazosimamiwa na Mamlaka kuhakikisha kwamba wanatimiza
wajibu wao wa kisheria na masharti ya leseni ili kuondoa usumbufu usio wa
lazima kwao na kwa watumiaji.
Inawezekana ikiwa kila mtu atatimiza
wajibu wake.
IMETOLEWA NA
Dr. Ally Y.
Simba
MKURUGENZI
MKUU
20 Januari, 2016
No comments:
Post a Comment