HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2016

TANZANIA YAICHAPATA SHELISHELI 3-0 KATIKA MASHINDANO YA VIJANA

 Golikipa wa timu ya taifa ya vijana ya Shelisheli, Gino Pleursuse akiusindikiza kwa macho mpira uliopigwa na Ibrahim Abdallah ukiingia wavuni wakati wa mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17. Mchezo huo ulifanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Serengeti Boys waliibuka na ushindi wa mabao 3-0. (Picha na Francis Dande)
 Ibrahim Abdallaha akishangilia baada ya kuipatia timu yake ya serengeti Boys bao la 2.
 Ibrahim Abdallah akimtoka beki wa Shelisheli, Juninho Mathiot.
 Mashabiki wa timu ya Srengeti Boys wakishangilia.
 Beki wa Serengeti Boys, Nickson Clement akimiliki mpira huku akizongwa na kiungo wa Shelisheli, Darren Dolley.
 Beki wa Serengeti Boys, Nickson Clement akitafuta mbinu ya kumtoka kiungo wa Shelisheli, Darren Dolley.

No comments:

Post a Comment

Pages