Na Mwandishi
Wetu
Chama Cha
kuogelea Tanzania (TSA), kinahitaji dola za Kimarekani 32,500 (Sh 71 milioni)
kwa ajili ya kuipeleka waogeleaji nane (8) wa timu ya Taifa kwenye mashindano
ya Dunia yaliyopangwa kufanyika mjini Windsor, nchini Canada.
Katibu Mkuu
wa TSA, Ramadhan Namkoveka alisema kuwa timu ya Taifa ya Tanzania inakuwa na
jumla wachezaji 11 ambapo kati ya hao, wachezaji watatu watalipiwa na
Shirikisho la Mchezo wa kuogelea duniani (Fina).
Namkoveka alisema kuwa kila muogeleaji anatakiwa
kulipiwa ni dola za Kimarekani 4,100 (Sh 8.2 million). Alisema kuwa TSA kwa
sasa haina fedha za kuweza kuwapeleka wachezaji wote hao kwa ajili ya
mashindano hayo.
Kwa mujibu wa Namkoveka, gharama kubwa
kuipeleka timu na kuwaomba wadau wa
mchezo huo kuwasaidia ili kuweza kufanikisha lengo lao ka kuipeleka timu hiyo
katika mashindano hayo.
“Tunahitaji
kupeleka waogeleaji wengi zaidi katika mashindano haya ambayo ni makubwa duniani,
mchezo wetu unakuwa kwa kasi na tunahitaji kupata waogeleaji wenye uzoefu
katika mashindano ya kimataifa,” alisema Namkoveka.
Alisema kuwa
TSA kimeunda kamati ya watu… kwa ajili ya kutafuta fedha kwa ajili ya
kuhakikisha timu hiyo inakwenda kwenye mashindano hayo.
Alisema kamati hiyo unaundwa na Mkurugenzi wa
Fedha wa TSA, Phillip Saliboko, Asma Hilal, Amina Mfaume (Mkurugenzi wa Ufundi
wa TSA), Inviolata Itatiro (Katibu Mkuu wa klabu ya Dar Swim Club), Geetha Prashant , Hamisi Mhini na Katibu Mkuu
wa klabu ya Dar es Salaam Swim Club (DSC), Inviolata Itatiro.
Wachezaji
waliochaguliwa kuunga timu hiyo ya Taifa ni Hilal Hilal, Aliasghar Karimjee,
Ammaar Ghadiyali, Denis Mhini, Adil Bharmal, Joseph Sumari ambao watashiriki kwa upande wa wanaume na kwa
upande wa wanawake ni Catherine Mason, Sylvia Caroiao, Sonia Tumiotto, Mariam
Foum na Magdalena Moshi.
No comments:
Post a Comment