HABARI MSETO (HEADER)


August 09, 2016

TEA YAWEZESHA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU SHULE YA SEKONDARI JANGWANI

NA IRENE MARK


MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA), imeahidi kusaidia mradi wa kukarabati  jengo la wanafunzi wenye mahitaji maalum na vifaa saidizi kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam. 

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Geraldine Mwanisenga alisema gharama ya mradi huo ni kuweka mazingira rafiki na bora ya kujifunza kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, ni sh. Milioni 130.4. 

Mbele ya Ofisa Ugawaji wa Rasilimali wa TEA, Anna Mlimuka na Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa mamlaka hiyo, Slyvia Lupembe, mwalimu Mwanisenga alionesha baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa kwa fedha hizo.

 Alivitaja baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa kuwa ni magongo ya kutembelea, kompyuta 20; mashine nne za kudurufu, magongo ya kutembelea pea tisa, baiskeli 9 za matairi matatu, kompyuta mpakato nne na projekta tatu za kufundishia wanafunzi wenye uoni hafifu.

 “Tunamahitaji mengi hasa kwa watoto wenye mahitaji maalum, changamoto kubwa ni vyoo na mabweni kwa ajili yao, hapa wapo mpaka wenye mtindio wa akili tunaletewa wanaofaulu kuingia sekondari,” alisema mwalimu Mwanisenga.

Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa TEA, Mlimuka alisema wataendelea kusaidia watoto hao kutokana na maboresho ya sheria ya uanzishwaji wamamlaka hiyo kuongeza na kukiwekea msisitizo kipengele cha elimu

maalumu.
Meneja Mawasiliano na  Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sylvia Lupembe (kushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa baiskeli tisa za walemavu Mkuu wa Shule ya Sekondari Jangwani, Geraldine Mwanisenga zilizotolewa na Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma shuleni hiyo. (Picha na Francis Dande)
Meneja Mawasiliano na  Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sylvia Lupembe akionyesha baadhi ya vifaa walivyokabidhi ikiwemo Kompyuta 20, printa 1, Laptop 4, Projector 3, Baiskeli 9, Magongo ya kutembelea, viatu maalum vya watu wenye ulemavu na vifaa vya kuongeza usikivu, meza na viti maalumu kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu.
Meneja Elimu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne Mlimuka (wa pili kushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa baiskeli za walemavu Mkuu wa Shule ya Sekondari Jangwani, Geraldine Mwanisenga zilizotolewa na TEA kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma shuleni hiyo
Makabidhiano ya Kompyuta.
Makabidhiano ya Magongo ya kutembelea watu wenye ulemavu.
Kutembelea Shule.
Kukagua Shule.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Tea, Silyvia Lupembe akisalimiana na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani.
Tabasamu.....Meneja Mawasiliano na  Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sylvia Lupembe akiwa amekumbatiana kwa furaha na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani.
Uongozi wa Tea na ule wa Shule ya Sekondari Jangwani wakikagua maeneo yatakayojengwa njia za walemavu wanaotumia baiskeli shuleni hapo.
Meneja Mawasiliano na  Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sylvia Lupembe (wa tatu kushoto) akionyesha sehemu ya vifaa walivyokabidhi kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Jangwanikwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu.

No comments:

Post a Comment

Pages