Na Bashir Nkoromo
Ofisa
Tawala wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo, pamoja na
mambo mengine, Mpogolo amewaasa Vijana wa Taasisi ya Vijana ya TYVA
kuhakikisha mipango yao ya kushirikisha Vijana katika shughuli za
kimaendeleo, inaendana na mipango ya serikali ili kuwezesha utekelezwaji
usiokinzana.
Amesema, iwapo TYVA itapanga
kwenye malengo yao mipango inayotofautiana na ile ya serikali kuhusu
maendeleo ya vijana na mengineyo, basi utekelezwaji wake unaweza kuwa
siyo rahisi kutokana na kukinzana kwa kuwa malengo ya serikali yatakuwa
yanaelekeza vingine wakati na wao wamelenga vingine.
Pia
aliwataka vijana wa TYVA na wengine kote nchini kuhakikisha wanailinda
amani ya Tanzania kwa gharama na nguvu zao zote, akitahadharisha kwamba,
amani ni tunu ambayo ikishapotea si rahisi kurejeshwa.
Ameitaka
TYVA na Taasisi ngingine za Vijana popote zilipo, kuhakikisha wanakuwa
makini dhidi ya watu wasioitakia mema Tanzania, akisema, wapo ndani na
nje ya nchi ambao hutamani sana kuona amani ya Tanzania inapotea au
inatetereka kwa namna yoyote, na kibaya zaidi kujaribu kujipenyeza kwa
makundi ya vijana ili kufanikisha azima zao mbaya.
"Kitu
kingine ninacho waasa wakati Taasisi yenu ya TYVA inatimiza miaka 16
sasa, waelimisheni vijana wenzangu, wajihadhari sana, wasije kutekwa na
watu waliopo ndani na nje ya Tanzania ili kuwatumia kuharibu amani ya
nchi yetu", alisema Mpogolo.
Baadaye
Mpogolo alizindua Kitabu cha Mipangokazi au bajeti ya Taasisi hiyo na
kukata keki kushiria TYVA kutimiza miaka 16 tangu ilipoanzishwa na
kuendelea kwa mafanikio kufanya kazi zake katika nyanja mbalimbali
ikiwemo kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa.

No comments:
Post a Comment