HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 16, 2017

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA ASHIRIKI KAZI YA UJENZI WA ZAHANATI YA UFYEMBA KATA YA WASA MKOANI IRINGA ILI KUHAMSHA ARI YAWANACHI KUFANYA KAZI ZA MAENDELEO

Na Erasto Chin’goro-WAMJW

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Bibi Sihaba Nkinga amewahamasisha wananchi kujitolea katika kutekeleza shughuliza maendeleo ikiwa ni sehemu ya kuhamsha ari wananchi kufanya kazi za maendeleo yao.

Ameyasema hayo katika ziara yake Mkoani Iringa wakati katika jitihada zake za kuhakakisha jamii inahuisha ari ya kushiriki shughuli za kujitolea na uanzishaji wa miradi inayoibuliwa na kutekelezwa na wananachi wenyewe kwa kushiriki kazi mbalimbali za utekelezaji wa shughuli hizo katika maeneo ya mijini na vijijini.

“Dhana ya maendeleo ya jamii inawataka wananachi kujitolea kushiriki kazi za maendeleo kwa kushirikisha kubaini mahitaji na changamoto zinazowakabaili wananachi na kujadiliana pamoja kuhusu mbinu za utatauzi wa changamoto hizo” alisema Bibi Sihaba.

Bibi Sihaba ameongeza kuwa wananchi waendelee kuainisha ushiriki wao katika kukamilisha miradi hiyo ya pamoja kwa kutumia rasilimali na nguzu kazi ya ndani badala ya kutegemea misaada ya nje ya jamii.


Aidha Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amewataka wananchi katika maeneo mengine kuiga mfano bora wa kijiji cha Ufyemba ili kujiletea maendeleo bila kusubiria msaada wa Serikali kuu.

Dhana hii ya kujitolea katika kutekeleza shughuli za maendeleo imefanikisha  kijiji cha Ufyemba kata ya Wasa kilichoko wilaya ya Iringa vijijini, mkoani Iringa kushirikiana na wananchi kukamilisha ujenzi wa zahanati ili kupata uhakika wa huduma za afya kwa watoto, wanawake, na jamii kwa ujumla.

Katika tukio hili, Katibu Mkuu aliongozana na uongozi wa mkoa wa Iringa ukiongozwa na KAtibu tawala Mkoa wa Iringa Bibi Wamoja Ayoub, viongozi wa wilaya ya Iringa vijijini, uongozi wa kata ya Wasa na kijiji cha Ufyemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ufyemba kata ya Wasa wilaya ya Iringa vijijini mkoa wa Iringa katika jitihda za kuhamasisha ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akihamasisha wananchi kuendeleza ari ya kushiriki kazi za maendeleo ya kijiji chao cha Ufyemba mkoani Iringa kwa kushirikiujenzia wa  zahanati hiyo ambayo unajengwa na wananchi wa kijiji hicho kwa kutumia nguvu za wananchi wenyewe ili kusogeza huduma za afaya kijijini.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinda akishirikiana na wakazi wa Kijiji cha ufyemba kubeba matofali katika kufanikisha ujenzi wa Zahanati kijiji cha Ufyemba kata ay wasa, iliyoko wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa.
Wananchi wa kijiji cha Ufyemba wakishiriki katika kubeba matofali na kujenga jingo la zahanati ya kijiji hicho ili kuondokana na taatizo la kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi mifuko 50 ya saruji kwa Mwenyekiti wa Kijij cha Ufyemba Bw Ronaganius Lunyungu ili kuunga mkono jitihada za wananchi hao katika kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ufyemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi pesa kwa Mwenyekiti wa Kijij cha Ufyemba Bw Roganius Lunyungu zilizopatikana katika harambee  ili isaidie katika kumalizia Ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ufyemba.

No comments:

Post a Comment

Pages