Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.
Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na baadhi ya Viongozi wa Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) akipoka bendera ya Taifa toka kwa Wanariadha Aphonce Simbu na
wenzake baada ya kuwasili toka nchini Uingereza kwenye Mashindano ya Marathon
ya 2017. (Picha na Maelezo).
Mwanariadha Alphonce Simbu akiwashukuru Viongozi mbalimbali
waliokuja kumpokea na kumpongeza kwa ushindi wake katika Mashindano ya Mbio
nchini Uingereza kwa mwaka 2017 ambapo aliweza kujinyakulia medali ya shaba.
Wazazi wa Mwanariadha Alphonce Simbu wakiwaonyesha Waandishi
wa habari (hawapo pichani) medali ya shaba aliyoshinda mtoto wao katika
Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017.
Mwanariadha Alphonce Simbu akiwaonyesha Waandishi wa habari
(hawapo pichani) medali ya shaba aliyoshinda katika Mashindano ya Mbio nchini
Uingereza kwa mwaka 2017.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na baadhi ya Viongozi wa Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) wakimpongeza Mwanariadha Alphonce Simbu kwa kuibuka mshindi wa tatu
ambapo alijinyakulia medali ya shaba. Hafla hiyo ilikuwa ni maalum ya kumpokea
yeye pamoja na wanariadha wengine wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
J.K Nyerere toka nchini Uingereza kwenye Mashindano ya Marathon ya 2017.
No comments:
Post a Comment