HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 01, 2017

MPIRA PESA FC MORNING STAR USO KWA USO MWAKAJOKA CUP

NA KENNETH NGELESI,TUNDUMA

TIMU  za soka za Morning Star na Mpira Pesa FC zote kutoka mjini Tunduma Mkoani Songwe Oktoba Mosi mwaka huu zitakutana kwa ajili ya kuwania Ubingwa wa kombe la Mbunge wa Jimbo hilo Frank Mwakajoka ‘Mwakajoka cup 2017’ utakao pigwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tuduma.

Akizungumza na Tanzania Daima jana Mjini Tunduma Kocha wa timu ya Mpira Pesa FC, Maisha Kyando alisema kuwa amekuwa akiwangalia  wapinzani wanavyo cheza hawana jipya na kwa jinsi alivyo kiandaa kikosi chake anaamini ubingwa kwa timu yake upo wazi.

‘Nawafahamu wapinzani wangu kikosi chao kiundwa na wazee hawawezi kukimbizana na vijana wangu wa Mpira Pesa FC na jinsi nilivyo jiandaa nina amini ubingwa ni wetu hawa Morning star hawana jipya  nina asilimia miamoja ya kubeba kombe  vijana wanajua kuwa Jumapili ni kazi hakuna ubishi ubingwa ni wetu’ alisema Kyando

Naye Rogadi Chuwa shabiki wa timu ya Mpira Pesa FC anasema kuwa wao ni watu wa vita hivyo hakuna ubishi timu yao itachukua Ubingwa wa Kombe la Mbunge  

‘Sisi kama mpira pesa ni watu wa vita tumejipanga kushinda kwani uwezo na sababu tunayo ya kushinda mchezo wa fainali na kuchukua Tunduma inajua kuwa timu Mpira pesa FC ndiyo timu pekee inayoundwa na vijana hata Mbunge mwenyewe anatajua kombe’ alisema Chuwa.
 “Sisi tumeshashinda kwani vijana wetu wanacheza mpira wa kitabuni mpira ulioenda shule hivyo, hiyo jumapili wapinzani wetu lazima wakae’ alisema Chuwa shabiki wa Mpira Pesa FC
Mwenyekiti wa Timu ya Morning Star Boniface Mwakabanje alisema kuwa timu yake italinyakua kombe hilo kwani klabu yake ina mipango ya mpira kwa muda mrefu na hawajaufanya mchezo huo kama ajali.

Sisi ‘Morning Star, Mpira ni sehemu ya maisha yetu  klabu yetu inawacheza wenye nidhamu ya soka wamekaa pamoja kwa muda mrefu wamejifunza mpira tofauti na timu zingine zimefanya kabumbu kama ajali mfano ni hawa Mpira pesa  FC wanacheza mpira baada ya wamesikia kuna mashindano’ alisema Mwakabanje

‘Morning star ni timu pekee katika Mji wa Tunduma na Mkoa wa Songwe kwa Ujumla na Tunduma  unapozungumzia vilabu wa mpiga wa miguu basi unaizungumzi timu hii ndiyo maana tunajiamini kubeba kombe’

Mwakabanje alisema ni maneno ya mdomoni kwani mpira ni vitendo uwanjani  kwani wanaitwa wazee ndiyo walioifikisha timu hiyo fainali za michuano hiyo iliyonza mapema Agost mwaka huu kwa kushikisha timu zaidi ya 30.

Alisema Monimng star ni timu pekee inayojua mpira katika Mji wa Tunduma ndiyo maana katika michuano hiyo kulikuwa na timu zaidi 30 zilikiundwa vijana lakini kwa kuwa wamefanya mpira kama ajali zilishindwa kufurukuta.

Mpira Pesa FC wametinga fainali hizo baada ya kuwafunga Serengeti FC kwa jumla ya bao 1-0 huku Morning Star wakiwafurumusha bila huruma Tunduma United bao 3-0 michezo yote ilipigwa katika dimba la Shule ya Msingi Tunduma.

Michuano hiyo itafikia tamati Oktoba Mosi ambapo bingwa ataondoka na kitita shi 500,000/,na kombe,mshindi wa pili sh.300,000/ ,mshindi wa tatu sh.200,000/ mshindi wa nne sh.100,000/ na fungaji bora ataondoka na kiatu. Mgeni rasmi anatazamiwa kuwa mbunge wa jimbo hilo Frank Mwakajoka.

No comments:

Post a Comment

Pages