Kamati ya Maadili ya TFF iliyokutana Jumamosi Novemba
3,2018 pamoja na mambo mengine ilipitia shauri linalomkabili Ndugu
Revocatus Kuuli (pichani), aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ambaye ameshtakiwa kwa
makosa matatu ya kimaadili.
2.0 TUHUMA ZILIZOWASILISHWA
Sekretarieti ya TFF iliwasilisha mbele ya Kamati mashtaka matatu (3) ambayo ni;
i).
Kusambaza nyaraka/barua za Shirikisho kinyume na ibara ya 12(1)(b) ya
Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya Mwaka 2013
(kama ilivyorekebishwa Mwaka 2015) na kinyume na kifungu cha
16(1)&(2) cha Kanuni za Maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) Toleo la 2013.
ii).
Kutoa maelezo yanayoonesha kuwa na mgongano wa maslahi kwa kuwapa watu
wasiohusika kinyume na kifungu cha 19(2) cha Kanuni za Maadili za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Toleo la 2013.
iii).
Kufanya vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho kinyume na ibara ya
50(1) ya Katiba ya TFF ya Mwaka 2013 (kama ilivyorekebishwa Mwaka 2015).
3.0 MAELEZO YA KOSA
Ndugu
Revocatus Kuuli kati ya tarehe 20 – 22 Septemba 2018, akiwa katika
nafasi yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) kwa makusudi na bila ya uhalali alitoa nyaraka
ya TFF kabla ya wakati wake ikiwa ni barua rasmi ya Shirikisho na
kuisambaza kwa watu wasiohusika.
4.0 SHAURI LILIVYOENDESHWA
Ndugu
Revocatus Kuuli alipelekewa hati ya mashtaka ili afike mbele ya Kamati
ya Maadili siku ya Jumamosi tarehe 3 Novemba 2018 saa 4.00 asubuhi
kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizoko
Uwanja wa Karume Ilala Dar es salaam. Hata hivyo Ndugu Kuuli hakufika
mbele ya Kamati na wala hakutuma taarifa ya kuomba udhuru, kama alikuwa
nao. Baada ya kupitia nyaraka na vielelezo mbalimbali, Kamati iliamua
kuendelea na shauri bila ya kuwepo Ndugu Kuuli, kwa kuwa katika wito
wake alielezwa kuwa Kamati itakuwa na haki ya kufanya uamuzi dhidi yake
endapo hatafika wala kutuma mwakilishi wa kumtetea.
Baada
ya kukubaliana kuendelea na shauri, Kamati ilitaka maelezo ya kina
kutoka Sekretarieti. Sekretarieti ya TFF iliieleza Kamati kuwa Kamati ya
Uchaguzi ya TFF chini ya uenyekiti wa Ndugu Revocatus Kuuli, ilifanya
kikao Dodoma Hotel siku ya Jumamosi tarehe 15 Septemba 2018 jijini
Dodoma. Katika kikao hicho, miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa, ni suala
la uchaguzi wa Simba ambapo Kamati ya Uchaguzi iligundua mapungufu
kadhaa. Klabu ya Simba ikaelekezwa, kupitia barua Kumb. Na.
DLM/LM.679/2018 ya tarehe 15 Septemba 2018, kuyafanyia marekebisho
mapungufu hayo ili yawasilishwe kwa ajili ya kupitishwa. Hata hivyo,
Ndugu Kuuli alianza kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa amesimamisha
uchaguzi wa klabu ya Simba huku akijua fika kuwa hayo si maamuzi ya
Kamati ya Uchaguzi.
Sekretarieti
ya TFF, baada ya kusikia taarifa hizo kwenye vyombo vya habari,
ilimwandikia Ndug Kuuli barua Kumb. Na. TFF/ADM/LM.748/2018 ya tarehe 19
Septemba 2018, kuomba ufafanuzi kama hayo anayotangaza kwenye vyombo
vya habari ni maamuzi ya kikao. Sekretarieti iliwasilisha mbele ya
Kamati ushahidi unaoonyesha kuwa barua hiyo ilipokelewa na Bi Mariamu
Mirambo, msaidizi wa Ndugu Kuuli, tarehe 20 Septemba 2018. Ndugu Kuuli,
badala ya kuijibu, aliisambaza barua hiyo kati ya tarehe 20 – 22
Septemba 2018 kwa watu ambao hawakuwa wahusika katika jambo hili wenye
anuani zifuatazo; michaelwambura5@yahoo.com na aden.rage@yahoo.com
bila kuwa na mamlaka wala idhini kutoka TFF. Sekretarieti iliwasilisha
ushahidi unaoonyesha kuwa mmoja wa watu waliotumiwa barua hiyo ni Ndugu
Michael Wambura, ambaye amefungiwa kutojihusisha na masuala ya mpira wa
miguu ndani na nje ya nchi maisha. Mwingine aliyetumiwa barua hiyo ni
Ndugu Aden Rage. Kitendo cha kuwatumia barua hiyo watu hao
kinadhihirisha wazi kuwa Ndugu Kuuli alikuwa na maslahi ya aina yake
katika suala hilo kwani watu hao waliwahi kuwa viongozi wa klabu ya
Simba katika nyadhifa mbalimbali kwa nyakati tofauti.
Pamoja
na Sekretarieti ya TFF kumuomba mwongozo kuhusiana na kusimamisha
uchaguzi wa Simba kupitia barua Kumb. Na. TFF/ADM/LM.748/2018 ya tarehe
19 Septemba 2018, Ndugu Kuuli hakujibu bali aliendelea kuongea na vyombo
mbalimbali vya habari huku akitumia lugha chafu na ya kashfa dhidi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Sekretarieti iliwasilisha
ushahidi mbele ya Kamati wa mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya
habari yakimnukuu Ndugu Kuuli akitoa maneno yenye kushusha hadhi ya
Shirikisho.
Baada ya kupitia shauri hilo, Kamati imemtia hatiani pasipo na shaka kwa makosa yote matatu (3).
5.0 HUKUMU
i). Shitaka la kwanza
Kamati
imejiridhisha kuwa Ndugu Revocatus Kuuli, aliyekuwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Uchaguzi ya TFF alisambaza barua (waraka) iliyotoka kwa Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) bila kuwa na
mamlaka wala idhini ya kufanya hivyo. Barua hiyo ilisambazwa kwa watu
wasiohukika huku mmoja wao akiwa amefungiwa kujihusisha na masuala ya
mpira wa miguu ndani na nje ya nchi maisha. Katika mahojiano na kituo
kimoja cha redio Ndugu Kuuli alikiri kuwa aliamua kuisambaza barua hiyo
kwa vile hakuuona usiri wowote kwani haikugongwa mhuri wa siri.
Kamati ilisikitishwa na kauli hiyo ya Ndugu Kuuli kwani akiwa kama kiongozi wa taasisi ya umma, alipaswa kufahamu kuwa barua na nyaraka ni siri za taasisi na hazitakiwi kusambazwa kwa wasiohusika. Aidha kwa nafasi yake kama wakili na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF alitegemewa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za Shirikisho.
Kitendo hicho ni kinyume na ibara ya 12(1)(b) ya Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya Mwaka 2013 (kama ilivyorekebishwa Mwaka 2015) inayosema “Every member of TFF shall have the following obligations; to be loyal to TFF, meaning, in particular, that members must abstain from any actions contrary to the interest of TFF” na kifungu cha 16(1)&(2) cha Kanuni za Maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Toleo la 2013 kinachotamka “(1) depending on their function, information of a confidential nature divulged to persons bound by this Code while performing their duties shall be treated as confidental or sectret by them as an expression of loyalty, if the information is given with the understanding or communication of confidentiality and is consistent with the TFF principles; (2) the obligation to respect confidentiaity survives the termaination of any relationship which makes a person subject to this Code”.
Kamati ilisikitishwa na kauli hiyo ya Ndugu Kuuli kwani akiwa kama kiongozi wa taasisi ya umma, alipaswa kufahamu kuwa barua na nyaraka ni siri za taasisi na hazitakiwi kusambazwa kwa wasiohusika. Aidha kwa nafasi yake kama wakili na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF alitegemewa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za Shirikisho.
Kitendo hicho ni kinyume na ibara ya 12(1)(b) ya Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya Mwaka 2013 (kama ilivyorekebishwa Mwaka 2015) inayosema “Every member of TFF shall have the following obligations; to be loyal to TFF, meaning, in particular, that members must abstain from any actions contrary to the interest of TFF” na kifungu cha 16(1)&(2) cha Kanuni za Maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Toleo la 2013 kinachotamka “(1) depending on their function, information of a confidential nature divulged to persons bound by this Code while performing their duties shall be treated as confidental or sectret by them as an expression of loyalty, if the information is given with the understanding or communication of confidentiality and is consistent with the TFF principles; (2) the obligation to respect confidentiaity survives the termaination of any relationship which makes a person subject to this Code”.
ii). Shitaka la pili
Kamati
imejiridhisha kuwa kitendo cha Ndugu Revocatus Kuuli, aliyekuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kutoa maelezo ya kusimamisha
uchaguzi wa klabu ya Simba kwenye vyombo mbalimbali vya habari huku
akituma nyaraka kutoka Shirikisho kwa waliowahi kuwa viongozi wa klabu
hiyo, kinaonyesha kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi. Aidha Ndugu Kuuli
alimtumia barua ya TFF Ndugu Michael Wambura kuhusiana na mambo ya mpira
huku akifahamu kuwa Ndugu Wambura amefungiwa kutojihusisha na masuala
ya mpira wa miguu ndani na nje ya nchi maisha. Kamati iliona kuwa
kitendo hicho cha Ndugu Kuuli kililenga katika kuvuruga amani
iliyokuwepo katika klabu ya Simba na kingeweza kusababisha vurugu katika
mpira wa miguu nchini.
Kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha 19(2) cha Kanuni za Maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Toleo la 2013 kinachosema “persons bound by this Code shall avoid any situation that could lead to conflicts of interest. Conflicts of interest arise if persons bound by this Code have, or appear to have, private or personal interests that detract from their ability to perform their duties with integrity in an independent and purposeful manner.
Private or personal interests include gaining any possible advantage for the persons bound by this Code themselves, their family, relatives, friends and acquaintances”.
Kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha 19(2) cha Kanuni za Maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Toleo la 2013 kinachosema “persons bound by this Code shall avoid any situation that could lead to conflicts of interest. Conflicts of interest arise if persons bound by this Code have, or appear to have, private or personal interests that detract from their ability to perform their duties with integrity in an independent and purposeful manner.
Private or personal interests include gaining any possible advantage for the persons bound by this Code themselves, their family, relatives, friends and acquaintances”.
iii). Shitaka la tatu
Kamati
imejiridhisha kuwa vitendo hivi vya Ndugu Revocatus Kuuli, vimeshusha
hadhi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa vile alikuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, ambayo ina jukumu la kusimamia
upatikanaji wa viongozi bora wa mpira wa miguu. Ndugu Kuuli alikaririwa
na kituo kimoja cha redio akisema kuwa hawezi kuhudhuria kikao cha
Kamati ya Maadili ya TFF kwa vile “…hizo ni tuhuma za kipuuzi zinazoweza
kufanywa na wapuuzi; mi siwezi kwenda kwenye kikao hicho nina kazi
nyingi za kufanya…” Pia alisisitiza kuwa hana mpango wa kuwa kiongozi wa
mpira wa miguu.
Kamati
ilijiridhisha kuwa Ndugu Kuuli alitumiwa wito kupitia barua Kumb. Na.
TFF/ADM/LM.791/2018 ya tarehe 29 Oktoba 2018. Barua hiyo ilitumwa kwa
njia za ems, barua pepe na WhatsApp. Kutokana na kauli zake, inaonysha
wazi kuwa Ndugu Kuuli alifanya vitendo hivyo kwa kudhamiria. Kitendo
hicho ni kinyume na ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF ya Mwaka 2013 (kama
ilivyorekebishwa Mwaka 2015) inayotamka kuwa “TFF members shall at all
times comply with the following ethical principles: (1) to behave
ethically and act with integrity in all situations, keeping in mind that
a reputation for integrity is of the utmost importance to TFF and its
objectives.”
Baada ya kujiridhisha kuwa Ndugu
Revocatus Kuuli amefanya makosa hayo, Kamati inamfungia kutojihusisha na
masuala ya mpira wa miguu ndani na nje ya nchi maisha. Adhabu hii
imetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 73(8)(b) cha Kanuni za Maadili ya
TFF Toleo la 2013, kwa kuzingatia uzito wa makosa yake, ambayo yangeweza
kusababisha vurugu na sintofahamu katika mpira wa miguu nchini.
Kamati
ilisikitishwa na kauli za kebehi, dharau na kashfa zilizokuwa
zikitolewa na Ndugu Revocatus Kuuli kupitia vyombo mbalimbali vya
habari. Kamati inaamini kuwa Ndugu Kuuli, akiwa kiongozi wa umma,
anawajibika kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kutoharibu
taswira ya utumishi wa umma mbele ya jamii. Kitendo chake cha kuita
tuhuma dhidi yake ni za kipuuzi na zinaweza kusikilizwa na wapuuzi siyo
tu kimeshusha hadhi ya Shirikisho bali pia kimeudhalilisha mpira wa
miguu. Aidha kwa nafasi yake kama wakili msomi, ilitarajiwa kuwa
anaelewa misingi ya utawala wa sheria; hivyo hakupaswa kuzungumza na
vyombo vya habari kwa lugha isiyopendeza na yenye maudhi; tena bila kuwa
na mamlaka ya kufanya hivyo. Kwa kuzingatia nafasi yake ya uongozi
katika utumishi wa Umma, Kamati inaiomba Sekretarieti ya TFF kuwasilisha
mbele ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, vielelezo vyote
vinavyoonyesha ukiukwaji wa maadili uliofanywa na Ndugu Revocatus Kuuli
ili ijiridhishe kama hakuna ukiukwaji wa maadili ya umma au uvunjaji wa
miiko ya uongozi.
6.0 HITIMISHO
Kamati
inalishauri Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuongeza
umakini wakati wa kufanya uteuzi wa viongozi wa Kamati mbalimbali ili
kuepuka watu wasio na maadili kupata nafasi nyeti zenye kufanya maamuzi
ya mpira wa miguu. Aidha Kamati inawaasa viongozi wa mpira nchini
kuzingatia mipaka ya kazi yao ili kuepuka mgongano na migogoro ya
kiutendaji. Vile vile viongozi wa mpira wa miguu wanashauriwa kuwa
makini wanapotoa kauli zao wakati wanazungumza na vyombo vya habari.





No comments:
Post a Comment