HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 08, 2019

LIVERPOOL YAPINDUA MEZA KIBABE, YAING’OA BARCELONA NA KUTINGA FAINALI


Messi akichuana na James Milner.


 Ni fainali ya tisa kwa Liverpool, ambako katika nane zilizotangulia, ilishinda na kutwaa taji mara tano (1977, 78, 81, 84 na 2005), huku ikipoteza fainali tatu (1985, 2007 na 2018), mbili kati ya hizo ikishinda kwa matuta. Inakuwa klabu ya nne Ulaya kufika fainali nyingi za michuano hii, nyuma ya Real Madrid (mara 16), AC Milan (11) na Bayern Munich (10)



LIVERPOOL, ENGLAND

USIKU wa Mei 7, 2019 huenda ndio usiku mbaya na mgumu kwa miamba ya soka la Hispania, FC Barcelona, baada ya ujikuta wakikumbana na kipigo cha ‘mbwa koko’ cha mabao 4-0 kutoka kwa Liverpool na kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL 2018/19).

Wakishuka dimba la nyumbani la Anfield, bila nyota wake ohamed ‘Mo’ Salah na Roberto Firmino, Liverpool hawakupewa nafasi yoyote ya kuing’oa Barcelona, lakini Majogoo wa Jiji hao wakatumia dakika 90 tu kupindua meza na kutinga fainali ya michuano hiyo. 

Barcelona walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutinga fainali ya michuano hii, itakayopigwa Juni 1 kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitan, jijini Madrid, Hispania, wakiongoza kwa ushindi wa mabao 3-0 walioupata katika pambano la kwanza Camp Nou. 

Haikuwa kama ilivyotarajiwa, Barcelona walipigwa hadi kuchakaa, kupitia mabao mawili mawili ya wakali wa Liverpool, Divock Origi na Georginio Wijnaldum, yaliyowapa tiketi ya kutinga fainali, wakisubiri dakika 90 za Ajax ya Uholanzi na Tottenham leo ili kujua mpinzani wao.

Origi aliitanguliza mbele Liverpool kwa kuifungia bao la uongozi mapema dakika ya saba na kudumu hadi mapumziko, mbele ya watazamaji 55,212.

Kipindi cha pili, mtokea benchi Wijnaldum, aliyejaza nafasi ya majeruhi Andy Robertson, alifunga mabao mawili ndani ya dakika mbili (yaani dakika za 54 na 56), kuipa Liverpool chini ya kocha Jurgen Klopp ushindi kama walioupata Barca nyumbani.

Origi, ambaye alipangwa kikosini kutokana na kuumia kwa Salah na Firmino (wanaomuweka benchi), aliimaliza kabisa Barcelona iliyokuwa na mastaa wao Lionel Messi, Luis Suarez na Philippe Coutinho, alipoifungia bao la ushindi lililoipeleka Liverpool fainali, kunako dakika ya 79.

Tottenham ya England, inaifuata Ajax leo usiku kwenye dimba la Amsterdam Arena, wakiwa na kibarua kigumu cha kuhitaji ushindi wa mabao 2-0 ili kutinga fainali, hii ni baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 katika mechi ya kwanza, ushindi unaowapa nguvu Ajax ya kusaka sare tu nyumbani.

Kikosi cha Liverpool na alama za ubora wao mchezoni: (4-3-3) Alisson 8; Alexander-Arnold 9, Matip 7.5, Van Dijk 9, Robertson 8 (Wijnaldum 46, 8.5); Fabinho 9, Milner 9, Henderson 9; Mane 9, Shaqiri 8.5 (Sturridge 90), Origi 9.5.

Kikosi cha Barcelona na alama za ubora wao mchezoni: (4-3-3) Ter Stegen 6; Sergi Roberto 6, Pique 7, Lenglet 6, Alba 6; Rakitic 6, Busquets 6.5, Vidal 6.5 (Arthur 75, 6); Coutinho 5.5 (Semedo 60, 6), Suarez 6, Messi 6.5.
Matokeo ya Liverpool yameibua mijadala miongoni mwa mashabiki wa soka duniani, kama tukio hili linaweza kuwa bora zaidi ya lile la kutoka nyuma kwa mabao 3-0 katika fainali dhidi ya AC Milan ya Italia, jijini Istanbul, Uturuki na kutwaa taji?

Wadadi na wachambuzi wa masuala ya soka, wanaamini hili ni zaidi ya lile, waibainisha kuwa Barcelona ni bora kuliko AC Milan. Lionel Messi ni bora zaidi kuliko Ricardo Kaka. Na hata Liverpool ya sasa ni bora kuliko Liverpool ile.
Daily Mail

1 comment:

  1. However, while employing a plumber, you should be a little careful regarding the example of the plumber for the reason that job is
    a part of lots of risks. So once you have to fix out your problem in connection with plumbing reputed companies are trustworthy.
    First, plan the amount storage space you will have to allot
    for each and every an affiliate the household.

    ReplyDelete

Pages