Kocha wa timu ya taifa Taifa
Stars Emmanuel Amuneke, ana matumaini kuwa bado timu yake ina nafasi ya
kufanya vizuri katika mchezo wa tatu wa mashindano ya Mataifa Afrika dhidi ya
Algeria,utakaofanyika Julai 1,katika Uwanja wa Al- Salam nchini Misri.
Akizungumza na waandishi wa
habari,Amuneke,alisema kuwa licha ya kuwa Algeria ina kikosi kizuri,lakini bado
ana matumaini makubwa na vijana wake kuwa watafanya vizuri katika mchezo huo wa
mwisho wa kundi C.
“Tumecheza na Algeria mara
kadhaa,nakumbuka mchezo wa Dar es Salaam tuliocheza tukafungwa bao mbili kwa
sifuri,na baadaye tukaja kucheza nao tukatoka nao 2-2,nakumbuka pia walikuja
wakatufunga bao 7 kwa bila,lakini hiyo yote ni historia,”alisema na kuongeza:
“Kwasasa hivi tunachokitazama
ni namna gani tutaweza kusawazisha makosa yetu yaliyotokea katika michezo
miwili iliyopita,na kufanya maamuzi sahihi tunapokuwa na mpira,kwahiyo Jumatatu
ni ukurasa mwingine na ni safari nyingine kwa Tanzania na Algeria,na hauwezi
kutabiri nani atakuwa mshindi,kwahiyo tutaingia uwanjani kupambana na kusaka
pointi tatu.”
Taifa stars,itashuka dimbani
kupambana na Algeria baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Senegal kwa bao
2-0 na mchezo wa pili dhidi ya Kenya ulioisha kwa Kenya kuibuka na ushindi wa
bao 3-2.
No comments:
Post a Comment