Na Mwandishi Wetu
Serikali kupitia Ofisi ya
Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na wadau
imedhamiria kuboresha huduma na upatikanaji wa vifaa saidizi kwa watu wenye
ulemavu.
Akizungumza wakati wa hafla ya
kupokea vifaa saidizi kwa ajili ya watu wenye ulemavu iliyoandaliwa na Kampuni
ya Sigara Tanzania (TCC Plc), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama alisema kuwa kundi la Watu wenye Ulemavu lilikosa baadhi ya fursa hapo
awali kutokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo.
“Tunafahamu watu wenye ulemavu
wanauhitaji wa huduma bora na vifaa saidizi vitakavyo wawezesha kumudu mazingira
ili nao waweze kujumuika katika nyanja zote,” alisema Mhagama
Alifafanua kuwa takwimu na
Sensa ya Taifa ya Watu wenye na Makazi ya mwaka 2012, imekadiria idadi ya watu
Tanzania ni zaidi ya milioni 44 ambapo milioni 2.5 ni Watu wenye Ulemavu.
Waziri Mhagama alisema, Serikali
imeazima kuboresha huduma kwa Watu wenye ulemavu ikimemo kutoa elimu bure na
kuimarisha elimu jumuishi, kujenga vituo vya afya na hospitali pamoja na utoaji
wa matibabu bure kwa watu wenye ulemavu wasio na uwezo.
Mbali na hayo, alihimiza wadau
pamoja na makampuni kuona umuhimu wa kuhudumia kundi la watu wenye ulemavu wakiwa
wanatoa huduma mbalimbali za kijamii.
Aidha, alipongeza Kampuni ya
Singara Tanzania (TCC) kwa msaada huo na kuwashauri waendelee kukumbuka kundi
hilo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Sheria na Uhusiano wa TCC, Bw. Godson Killiza alisema kuwa watu wenye ulemavu wana
uwezo mkubwa na nijukumu kama wadau kuwasaidia na kuwaunga mkono kwenye masuala
mbalimbali.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho
la Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bi. Ummy Nderiananga alieleza kuwa juhudi za
Serikali katika kushirikiana na wadau itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa
changamoto za Watu wenye Ulemavu katika kufanikisha masuala yao.
No comments:
Post a Comment