Na Tatu Mohamed
JUMLA ya wanafunzi 208 wamehitimu mafunzo ya mfumo wa kutumia Mtandao kupitia maombi ya 'Visomo' yanayotolewa na Chuo cha Kipawa jijini Dar es Salaam kilichopo chini ya Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Mfumo
huo unaopatikana bure kupitia programu ya Visomo unamuwezesha
mwanafunzi kusoma kupitia picha pamoja na maandishi na baadae kufanya
mtihani.
Akizungumza
katika maonesho ya 43 kimataifa ya biashara ya Dar es salaam (DITF),
yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Mratibu wa
mradi wa Visomo Charles Mapuli (pichani), amesema katika mfumo huo wa visomo kuna
jumla ya kozi 13 zilizogawanyika katika mada 4. hivyo mwanafunzi
atapaswa kuchagua anayoitaka.
"Baada
ya kuchagua kozi anayoitaka na kulipia mwanafunzi atapewa tokeni ili
aweze kuona mafunzo hayo na mwisho wa siku atapewa mtihani wenye mfumo
wa jibu sahihi au sio kweli," amesema Mapuli.
Amesema
mradi huo ulianza mwaka 2016 ambapo mpaka sasa upo katika awamu ya pili
ukiwa umebuniwa na Chuo Cha Veta kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya
mkononi ya Airtel.
"Mpaka Sasa jumla ya watu elfu 43 wamefungua aplikesheni hii ya visomo na elfu 13 wamejisajili "alisema Mapuli
Ameongeza kuwa mfumo hautumii intaneti pale msomaji anapokuwa akisoma na upo katika mfumo wa lugha ya kiswahili na kingereza.
No comments:
Post a Comment