HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2019

Teknolojia ya kibao cha kufulia nguo inavyowavutia wananchi sabasaba

Na Janeth Jovin

MAMLAKA ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),  imetambulisha teknolojia mpya ya Kibao cha kufulia nguo za aina zote kwa urahisi na kwa haraka inayoonekana kuwavutia wananchi mbalimbali.

Teknolojia hiyo mpya  iliyoletwa nchini na raia wa Japan, Ryuta Okamoto (pichani), inaelezwa kuwa itawakomboa wanawake wengi na watoto katika kazi za kufua nguo kwa kutumia mkono.

Akizungumza  leo jijini Dar es Salaam wakati wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara yaliyoanza ramsi Juni 28 mwaka huu,  Okamoto ambaye ni Ofisa maendeleo anayefanya kazi katika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma kwa kujitolea kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA),  anasema teknolojia hiyo ya kutumia kibao  ilianzia bara la Ulaya kisha kwenda nchini Japan barani Asia.

Anasema alijifunza kutengeneza teknolojia hiyo kutoka kwa bibi yake na kwa sasa wajapan wengi wanatiumia, anaamini kuwa ujio wa teknolojia hiyo hapa nchini itawavutia watanzania ambao waanza kuitumia na kuokoa muda mwingi wakati wa ufuaji.

Okamoto anasema teknolojia hiyo inamuwezesha mtu kufua nguo moja kwa nusu dakika hivyo uokoa muda na kumrahisisha mtu kumaliza kazi ya kufua kwa haraka kisha kuendelea na shughuli zingine.

"Kibao hiki kinapatikana hapa Sabasaba kwa Sh. 5000 na kazi ya kuvitengeneza inafanywa na wanafunzi wa Chuo cha VETA kutoka Songea wanaosomea kozi ya useremala, " alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages