Na Mwandishi Wetu, Katavi
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewataka wakulima na wadau mbalimbali katika sekta hiyo na mifugo hapa nchini kuchangamkia
fursa ya mikopo inayodhaminiwa na benki hiyo kupitia mabenki ya biashara kuongeza uzalishaji.
fursa ya mikopo inayodhaminiwa na benki hiyo kupitia mabenki ya biashara kuongeza uzalishaji.
Akizungumza katika kikao ch wadau wa kilimo mkoani Katavi hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (pichani), alisema walikulima wanapaswa kuchangamkia fursa za mikopo katika mabenki hayo ambayo ni mkombozi na pia zitasaidia kuchagiza ukuaji wa sekta ya viwanda.
“Benki ipo tayari kutoa mikopo kwa haraka katika miradi mbalimbali itakayosaidia wakulima wadogo kukua, hivyo nawaomba wadau waandae maandiko na kuyawasilisha TADB kwa ajili ya utekelezaji wa haraka,” alisema Bw.Justine na kuzitaja benki ambazo TADB inadhamini mikopo kwa wakulima ni pamoja na NMB, CRDB na TPB. Aidha katika kikao hicho na wadau wa kilimo, Bw.Justine mbali ya
kutembelea maeneo yenye viwanda alipata kusikia changamoto ambazo wakulima wanakabiliana nazo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi na kuongeza tija katika kilimo.
kutembelea maeneo yenye viwanda alipata kusikia changamoto ambazo wakulima wanakabiliana nazo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi na kuongeza tija katika kilimo.
Kuhusu kufufua kiwanda cha Alizeti kilichopo Wilaya ya Tanganyika mkuoni humo, Bw.Justine alisema benki itakaa na wadau mbalimbali kutengeneza muundo wa ukopeshaji na kuainisha mkopaji ambaye atakuwa tayari kuwekeza katika kiwanda hicho.
“Mkoa wa Katavi una fursa nyingi za uwekezaji katika viwanda vya nyama, maziwa kutokana na uwepo wa ngombe pia kuendeleza kiwanda cha kusindika asali ambayo hupatikana kwa wingi mkoani humu,” alisema Bw.Justine.
Alisema Katavi ina mazao ya kipaumbele kama vile tumbaku, pamba, korosho, kahawa na chikichi hivyo uwekezaji katika kukuza uzalishaji katika mazao hayo na uanzishwaji wa viwanda kutainua uchumi katika mkoa na kufanikisha azma ya serkali ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025 kufikiwa kwa vitendo. “TADB ipo kwa ajili ya watanzania wote hivyo ni wajibu wa kila mtu katika eneo lake kuandaa andiko la mradi na kuwasirishwa kwetu kwa ajili ya hatua mbalimbali ili kutoa mikopo kwa jamii itakayosaidia kuendeleza sekta ya kilimo na mifuko nchini,” alisema.
Alifafanua kuwa benki hiyo inawataalum wakutosha ambao wapo tayari kutoa elimu ya namna ya kuandaa maandiko ya mradi kitaalum ili yatakapo wasilishwa kusiwe na kipingamizi katika andiko na kupelekea mkopo kutoka kwa haraka. Bw.Justine alieleza kuwa katika kuchagiza maendeleo ya nchini kupitia kilimo, mifugo na uvuvi benki yake itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha huduma ya mikopo inawafikia walenga kwa haraka zaidi ili kufikia malengo ya kuinua uchumi wa nchi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa Katavi, Bw.Juma Homera mbali ya kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa TADB kwa kuitikia mwaliko wa kutembelea mkoa huo na kujionea fursa zilizopo, aliainisha changamoto zilizopo mkoani hapo ikiwemo upungufu wa viwanda vya kusinda mazao mbalimbali ili kuongeza thamani.
“Kazi kubwa iliyopo ni kuunganisha wadau kutokaSerikali na Sekta binafsi na wote ndani ya mkoa ili kuweka mikakati ya pamoja kutatua changamoto mbalimbali zilizopo ili kuleta tija katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi,” alisema Bw. Homera Alisema anaamini katika ushirikiano wa kila mmoja katika nafasi kutekeleza majukumu yake ili malengo na mikakati ya mkoa iwekeze kutekelezeka na kuchochea ukuaji wa uchumi katika mkoa na taifa kwa ujumla wake.
No comments:
Post a Comment