HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 06, 2019

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada Mkoani Songwe katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

Wananchi wakipata huduma za usajili wa vitambulisho vya Taifa katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa vipeperushi na vitabu  mbalimbali vya Elimu ya mawasiliano kwa Wananchi mkoani Songwe katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada inayofanyika katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.
Wananchi wakisoma kitabu cha Muongozo wa Mawasiliano cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
 Wananchi wakipata huduma za usajili wa vitambulisho vya Taifa katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.
ananchi wafurika katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada inayofanyika Nyanda za Juu Kusini katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.


Na Mwandishi Wetu

Wakazi wa Mkoa wa Songwe  na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Mkuu wa nyanda ya Juu Kusini Kaskazini wa TCRA  Mhandisi  Asajile John amesema ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe katika Soko la Mlowo na viunga vyake  kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano.
John amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

John amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

John amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.


Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Mhandisi John amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

John amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

"TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema John

No comments:

Post a Comment

Pages