SHIRIKISHO
la Soka Ulimwenguni (FIFA) limemnyuka aliyekuwa Rais wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi kifungo cha miaka 10 kutojihusisha na
Soka sambamba na faini ya zaidi ya Bilioni 1, baada ya kumkuta na hatia
ya matumizi mabaya ya fedha na kughushi nyaraka.
Mbali na adhabu hiyo, Malinzi pia amepigwa faini ya Dola za Kimarekani 503,000 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.1 za Kitanzania.
Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Maadili ya FIFA baada ya uchunguzi uliobaini kuwa Malinzi alihusika katika matumizi mabaya ya fedha za FIFA (FIFA Financial Assistance Programme (FAP) funds), fedha za CAF, fedha nyingine za TFF pamoja na kughushi nyaraka za maazimio ya Kamati ya Utendaji ya TFF kati ya mwaka 2013 na 2017.
Adhabu hiyo inaanza kufanya kazi kuanzia Novemba 8, 2019 na tayari Malinzi mwenyewe ameshajulishwa.
“Kamati imemkuta na hatia ya kuvunja kanuni ya 24 inayohusu kughushi nyaraka, na kanuni ya 28 inayohusu matumizi mabaya ya fedha katika kanuni za maadili ya FIFA toleo la mwaka 2018 na hivyo inamfungia miaka kumi kujihusisha za shughuli zote za soka Kitaifa na Kimataifa”, imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa leo na FIFA.

No comments:
Post a Comment