Na Mwandishi Wetu
WACHUNGAJI
watatu wa mifugo, wamehukukiwa kifungo cha miezi sita au kulipa faini
ya shilingi laki mbili kwa kosa la kujeruhi walinzi wa Msitu wa Hifadhi
ya Kohondo uliopo kijiji cha Kihondo kata ya Doma wilaya ya Mvomero
mkoani Morogoro.
Wachungaji hao waliohukumiwa ni
Sperwa Kishakwii, Daniel Babalai na Kashuma Kishaki.
Hukumu
hiyo imetolewa Novemba 6/2019 na Hakimu Mussa Lilingani baada ya
kusikiliza ushahidi wa pande zote ambapo Mahakama imewakuta na hatia
wafugaji hao watatu.
Wafugaji
hao wanakutwa na hatia baada ya kuwashambulia na kuwajeruhi walizi
wawili wa kamati ya Ulinzi wa hifadhi ya asili ya Msitu wa kijiji cha
Kihondo, Emmanuel Willnely na Every Pius wakitaka kukomboa mifugo
iliyokuwa ikishikiliwa.
Lilingani
alisema hoja zilizo wasilishwa na watuhumiwa mahakamani hapo pamoja na
mashahidi wao zilikosa uthibitisho ikiwemo kudai walipo fika kituo cha
Polisi Doma waliwekwa Rumande bila Kuhojiwa, Umri walieleza kuwa chini ya
Miaka 18 sambamba na maelezo kuwa siku hiyo ya tukio sio wao waliokuwa
wakichunga mifugo iliyo kamatwa.
"Kufuatia
ushahidi uliowasilishwa na upande wa walalamikaji pamoja na vielelezo
vya upelelezi vya Jeshi la Polisi mahakama imejiridhisha na ushahidi
ikiwemo vielelezo vya matibabu PF3, Fomu ya maelezo ya onyo toka kituo
cha Polisi Doma pamoja na mkataba wa makabidhiano ya mifugo iliyo
kamatwa wafugaji walikuwa na hatia" alisema.
Hakimu
Lilingani aliwaeleza washtakiwa hao kuwa mahakama imewatia hatiani na
kuwataka kila mmoja kuieleza mahakama kama anautetezi wowote ili
apunguziwe adhabu.
Mtuhumiwa
namba moja Sperwa Kishakwii akatumia muda huo kuieleza mahakama kazi
yake ni Mchungaji na anafanya kazi hiyo kama kibarua, hana baba wala
mama anawadogo zake watatu na mmoja anaumwa, huku mtuhumiwa namba mbili
yeye hakuwa na utetezi.
Katika
utetezi wake mtuhumiwa namba tatu Kashuma Kishaki ameieleza mahakama
kuwa kazi yake ni Mchungaji wa mifugo hana baba na mama yeka haoni, ana
wadogo zake watatu, wawili ni wanafunzi na mmoja hana akili timamu hivyo
yeye ndie tegemezi katika familia yao.
Mbali
na utetezi huo Hakimu Lilingani alisema watuhumiwa wote wanahukumiwa
kama watu wazima na kwakua wote hawajawai kuwa na kosa linguine kabla,
adhabu ya mahakama ni kwenda jela miezi sita ama kulipa faini kiasi cha
Shilingi Laki mbili kwa kila mmoja pamoja na Fidia ya Shilingi laki
mbili kwa ajili ya waliojeruhiwa.
Pamoja
na hayo mahakama imetoa amri kutaka fedha za adhabu zilipwe ndani ya
siku 45 na kiasi kingine cha fedha za fidia zilipwe ndani ya siku tano
baada ya fedha za mahakama.
Kwa
mujibu wa hakimu Lilingani Rufaa ya kesi hiyo ipo wazi ndani ya kipindi
ca siku 30 huku nje ya mahakama walalamikaji wakieleza kuto ridhishwa
na hukumu iliyo tolewa.
No comments:
Post a Comment