HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 04, 2019

PROF. NDALICHAKO AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA



Skauti Mkuu wa Tanzania, Mwantumu Mahiza, akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Desemba 4, 2019.

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania.

Wajumbe wa mkutano mkuu wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani).

Wajumbe wa Bodi.

Mkutano ukiendelea.
 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Desemba 4, 2019.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, akipongezwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, baada ya kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania.

Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti, Grace Kado, akimkabidhi zawadi ya picha ya mwazilishi wa Skauti duniani, Baden-Powell, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Desemba 4, 2019.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ambaye pia ni Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania, akipokea zawadi ya picha ya Baden-Powell ambaye ni mwanzilishi wa skauti duniani kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ambaye pia ni Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania, akipokea zawadi ya picha ya mwanzilishi wa skauti duniani, Baden-Powell, kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako.

Meza Kuu.

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi.

Picha ya pamoja.


Picha ya pamoja.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ambaye pia ni Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania, baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania.
Skauti kutoka Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere wakiimba ngojera katika mkutano huo.

Skauti wakicheza na kuimba nyimbo za kitamaduni.




Na Asha Mwakyonde

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, amekitaka Chama cha Skauti Tanzania kuanzisha miradi ya kilimo cha mboga mboga kwa lengo la kuinua kipato na kuwawezesha vijana wa chama hicho kuwa na uelewa wa kufanya kazi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Desemba 4, 2019, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho amesema uanzishwaji wa mradi huo utawajengea vijana hao utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii.

Prof. Ndalichako amesema uongozi wa chama hicho ukiwa na ubunifu na nia thabiti ya kukabiliana na changamoto hakika vijana watajifunza mambo na namna ya kujenga taifa lao kwa ari moja.

"Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuwafundisha vijana hao namna ya kuwapatia elimu ambayo inawafanya watambue mambo ambayo hayafai katika taifa hili likiwamo suala la rushwa," amesema Prof. Ndalichako.

Aidha amewataka wazazi na walezi kuwaruhusu watoto wao kujiunga na chama hicho ambayo kimekuwa kikiwafundisha vijana maadili mema na kupinga rushwa.

Awali Mkuu wa Skauti Tanzania, Mwantumi Mahiza, amesema kuwa katika ili kutatua tatizo la rushwa nchini hasa kwa kuwaandaa vijana tayari wameingia makubaliano na Taasisi ya kuthibiti na kupamba na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), kutoa elimu kupitia skauti katika shule za msingi na sekondari nchini.

" Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2019 kutoka Wizara ya elimu tunazo jumla ya shule za msingi za serikali na binafisi ni 17,804 zenye wanafunzi 10,617,373,amesema Mwantumu.

Ameongeza kuwa wanazo shule za sekondari za serikali na binafisi kidato cha kwanza hadi cha nne zipatazo 5,716 zenye jumla ya wanafunzi 2, 595,902 na kwamba wanatarajia kuwafikishia elimu hiyo juu ya madhara ya rushwa na namna ya kupambana nayo wanafunzi hao 13,213,275.

Amesema kuwa lengo la chama hicho ni kuisaidia jamii ya Watanzania kuwa na vijana wazalendo wenye uchungu na nchi yao na kwamba kupitia skauti watajenga Taifa lenye vijana mahiri wenye weledi wakutosha na waadilifu kwa nchi yao.


No comments:

Post a Comment

Pages