HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 04, 2019

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada wilayani Babati katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

 Bibi zetu ambao wamezaliwa mapacha  wamejitokeza  kupata namba zao za vitambulisho vya Taifa  (NIDA) na kisha kujisajili kwa njia ya alama za vidole.
 Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Emelda Salum akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara wa Katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi ya Magugu ya usajili wa Laini za Simu kwa Alama za vidole.
 Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa maelezo kwa Wananchi wa Babati.
 Mwananchi akisajili laini ya simu kwa alama za vidole moja ya Kampuni ya huduma za Simu za Mkononi wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.
Wananchi wakipata huduma ya usajili wa Laini za simu wakati Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.


Na Mwandhi Wetu

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada wilayani Babati  katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole.


Wakazi wa wilayani Bahati  mkoani Manyara  na viunga vyake  wamejitokeza katika kupata namba za vitambulisho vya Taifa ili kukidhi matakwa ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA ipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya  Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole na kuongeza kuwa ambaye hatatimiza matakwa ya kisheria ya kusajili laini ya simu kwa alama za vidole laini hiyo  itafungw


Kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika maeneo ya miji na Mkoa lengo Wananchi kutumia fursa ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole ambayo unakwenda nchi nzima

Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Babati katika Stendi ya mabasi ya Zamani ya Magugu Mkuu wa Kanda ya Kasikazini wa  TCRA  Mhandisi Emelda Salum amesema ni fursa kwa wananchi wa Babati  na maeneo Mbalimbali wamefika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya Magugu kupata namba ya kitambulisho cha Taifa katika mfumo wa NIDA na kuweza kusajili laini ya simu kwa alama za vidole.

 Mhandisi Salum Amesema katika Kampeni hiyo imekuwa inafanywa na kanda hiyo ikiwa  kila mwananchi aweze kuwa na namba ya Kitambulisho au Kitambulisho cha  Taifa  kutokana Ushirikiano na NIDA kuwa katika Kampeni hiyo.

 
Amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa kwa pamoja  kwa huduma za mawasiliano na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika  huduma  za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda ulioabakia ni 27 mdogo hivyo kila mtu atumie kutafuta taarifa zinazokidhi usajili wa laini kwa alama za vidole.


Hata hivyo amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Hata hivyo amesema kuwa
 kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana  makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.

 Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia wananchi kuhakikisha kila mwananchi anasajili laini  ya simu kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa au namba ya kitambulisho hicho.

Salum  amesema kuwa  TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa kupitia Kampeni ya Mnada kwa mnada.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze  kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31 kwa kufika katika maduka  ya watoa huduma wa Kampuni za Simu za Mkononi.

"TCRA tutahakikisha tunawafikia  wananchi wote kupata  elimu ya  utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema Mhandisi Salum.

Ameongeza kuwa  Kampeni iko katika mikoa yote iliopo katika kanda ya Kaskazini.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA  Makao Makuu Mabel Masasi amesema kuwa wananchi wameitikia kwa kujitokeza kwa wingi  kuangalia namba  vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole na wengi wamepata namba hizo  na kufanya usajili kwa watoa huduma wa Kampuni za Simu za Mkononi.

Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata utaratibu wa  vitambulisho vya Taifa.

No comments:

Post a Comment

Pages