Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Hospitali ya Rufaa ya Kusini wakati wa
ziara yake ya siku mbili mkoani Mtwara kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evord Mmanda.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Msajili wa Hati Kanda ya Kusini Mpoki Mwalufunda katika halmashauri ya Nanyamba jana wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Mtwara kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evord Mmanda. (Picha na Munir Shemweta, Wizara ya Ardhi).
Na Munir Shemweta, WANMM MTWARA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Msajili wa Hati Kanda ya Kusini Mpoki Mwalufunda katika halmashauri ya Nanyamba jana wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Mtwara kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evord Mmanda. (Picha na Munir Shemweta, Wizara ya Ardhi).
Na Munir Shemweta, WANMM MTWARA
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameonesha kutoridhishwa na
utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani
Mtwara na kuagiza kuondolewa katika nafasi ya mkuu wa idara ya ardhi wa
halmashauri hiyo Mariam Kimoro.
Uamuzi wa kumvua wadhifa
wa ukuu wa idara ya ardhi katika
Manispaa ya Mikindani unafuatia Mkuu huyo wa idara kushindwa kusimamia vyema ukamilishaji
wa hati za ardhi 150 zilizoombwa na wamiliki wake kwa miaka tofauti kuanzia
mwaka 2011.
Akizungumza katika
manispaa hiyo jana wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Mtwara Dkt Mabula
alisema haiwezekani hati za ardhi kuandaliwa tangu mwaka 2011 ambapo hadi sasa
wamiliki wake wameshindwa kusaini kwa ajili ya kumilikishwa jambo alilolieleza
linaikosesha pia serikali mapato.
‘’ Hatuwezi kuwa na Mkuu
wa Idara asiyefanya kazi yake ipasavyo, anasubiri watu waje wasaini na hakuna
jitihada zozote zilizofanyika kuwatafuta mmiliki wake na hata kuwapigia simu?’’
alisema Mabula.
Afisa Ardhi wa Manispaa
ya Mtwara Mikindani Edna Chacha aliitetea idara hiyo kwa kueleza kuwa imekuwa
ikifanya juhudi mbalimbali za kukamilisha hati za ardhi lakini changamoto kubwa ni wamiliki wake kushindwa kujitokeza
kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kumilikishwa.
Hata hivyo, Naibu Waziri
Mabula alipingana na Afisa Ardhi huyo kwa kumueleza kuwa haiwezekani idadi ya
wamiliki 150 kwa pamoja washindwe kupatikana kwa ajili ya kusaini ili
wamilikishwe na kubainisha kuwa hali hiyo inachangiwa na uzembe wa idara hiyo kushindwa
kuwafuatilia wamiliki hao
Dkt Mabula ambaye
aliitembelea pia halmashauri za Mtwara na Nanyamba amezitaka idara za ardhi kwenye
halmashauri za mkoa wa Mtwara kujipanga katika kushughulikia masuala ya ardhi
ikiwemo kuingiza majalada ya ardhi kwenye mfumo wa kielektroniki kwa asilimia
mia moja.
Katika
hatua nyingine, Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameridhishwa
na maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo eneo la
Mitengo katika mkoa wa Mtwara.
Ujenzo huo unaotarajiwa
kukamilika mwishoni mwa mwaka huu na kugharimu takribana bilioni 15.8 unafanywa
na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na utahudumia mikoa ya kusini ya Mtwara,
Songea, Lindi pamoja na nchi jirani ya Msumbiji.
Akizungumza wakati wa
ukaguzi wa jengo hilo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
amelipongeza shirika la Nyumba la Taifa kwa kujenga jengo hilo kwa kasi
aliyoieleza kuwa italifanya jengo kukamilika kabla ya muda uliopangwa.
Kwa upande wake Meneja wa
Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mtwara Angelina Magazi alisema Shirika lake
limejipanga kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilika mapema na kubainisha
kuwa ujenzi huo kwa sasa unafanyika usiku na mchana.
‘’ Lengo la kufanya kazi
usiku na mchana ni kuhakikisha tunakamilisha ujenzi wa jengo hili la hospitali
ya Rufaa ya Kanda ya Kusini mapema kabla ya muda tuliopewa kwani hayo ndiyo
malengo yetu ya ndani kama Shirika’’ alisema Magazi.
No comments:
Post a Comment