Kiwanda cha Maziwa Karatu Kilichohujumiwa na Wajanja wachache.
Na Bryceson Mthias, Karatu
WANANCHI wa Wilaya ya Karatu mkoani
Arusha, wamezidiwa na furaha baada ya kuwepo kwa tetesi za kurejeshwa kwa Kiwanda
cha Maziwa cha Ushirika wa Ayalabe Dairy
baada ya fedha zao kuhujumiwa na Wajanja wachache.
Waliofurahishwa
na tetesi hizo ni pamoja na wafugaji waliokuwa wakikamua na kuuza maziwa kiwandani
na kujipatia kipato wakiwemo wachuuzi na wafanya biashara ya maziwa sehemeu mbalimbali.
Fununu
za kurejeshwa kwa Kiwanda hicho katika kazi zake zinadaiwa zinafuatia agizo la Waziri
wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), ambaye Novemba 10, 2019 aliagiza viongozi wote
wa Chama hicho kukamatwa kutokana na ubadhirifu wa fedha.
Pamoja
na kuwepo kwa taarifa za watuhumiwa hao kupata dhamana kutolewa rupango,
wananchi hao wamedai wamehemewa na furaha kwa sababu kuna fursa tena ya kuwepo
kwa ajira na kukuza kipato chao
Novemba 10, 2019 akiwa
kwenye ziara ya kikazi, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb) mara baada ya
kusikiliza malalamiko ya wanachama wa Chama hicho kwenye kikao kazi
kilichofanyika uwanja wa Chama, aliagiza Jeshi la Polisi, Mkuu
wa Upelelezi Arusha kwa
kushirikiana na TAKUKURU kuwakamata watuhumiwa.
Waziri
Hasunga aliagiza viongozi hao kukamatwa haraka iwezekanavyo kwani dhamira ya Serikali
ya awamu ya tano ya kuanzisha vyama vya Ushrika ilikuwa ni kuwanufaisha
wananchi kupitia umoja huo.
Waziri Hasunga pia aliagiza kukamatwa kwa viongozi
wote wa makampuni yaliyochukua hela kinyume na taratibu za ushirika, na katika
hatua nyingine aliagiza mtu mmoja jina linahifadhiwa (Blanka Michael) akamatwe
kutokana na kukodisha eneo la Chama cha Ushirika wa Ayalabe Dairy pasipo
kufuata utaratibu wa kisheria.
Aidha katika mkutano huo pia Waziri Hasunga aliagiza
kuwekwa kizuizini viongozi na wajumbe wa kamati ya usimamizi wa Chama cha Akiba
na mikopo cha Ayalabe Majina yao yamehifadhiwa (ni aliyekuwa Mwenyekiti Ndg
Lazaro Titus Lazaro na wajumbe Joseph Bayo na Eudesi Jonas).
No comments:
Post a Comment