HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 13, 2020

KOCHA MPYA YANGA ALA KANDARASI YA MWAKA NA NUSU

Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Ubelgiji, Luc Eymael (kulia) na Riedoh Berdien, kocha Msaidizi na viungo wakionyesha mkataba wa mwaka mmoja na miezi sita kuitumikia klabu hiyo.

Na Mwandishi Wetu

HATIMAYE, LUC Eymael Kocha Mkuu wa Yanga, raia wa Ubelgiji na Riedoh Berdien, Kocha Msaidizi na viungo wameingia mkataba wa mwaka mmoja na miezi sita kuitumikia Yanga.

Eymael amejiunga na Yanga akichukua mikoba ya Mwinyi Zahera ambaye alitimuliwa ndani ya kikosi hicho kutokana na kuwa na matokeo mabovu ndani ya Yanga.


Leo, Mbelgiji huyo alianza kazi na kikosi chake hicho kinachojiaanda kumenyana na Kagera Sugar, Jumatano mchezo wa ligi.

No comments:

Post a Comment

Pages