Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Kising’a mkoani Iringa wakati alipofanya ziara kijijini hapo
kuangalia vikundi vya malezi vinavyosaidia kupambana na vitendo vya ukatili
dhidi ya wanawake na watoto.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza mara baada ya
kukabidhi mabati 20 kwaajili ya kupaua jengo la kukamua mafuta ya Alizeti
kijijini hapo wakati alipofanya ziara kuangalia vikundi vya malezi vinavyosaidia kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya
wanawake na watoto.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipanda mbege ya mahindi
katika Shamba la kikundi cha Malezi cha kijiji cha Kising’a kwa ajili ya
kuwezesha watoto walio katika mazingira magumu kijijini hapo wakati alipofanya
ziara kijijini hapo kuangalia vikundi vya malezi vinavyosaidia
kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. (Picha na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WAMJW).
Na Mwandishi Wetu, Iringa
Mkoa wa Iringa kwa kipindi cha Januari mpaka
Novemba 2019 umekuwa na matukio takribani 404 ya vitendo ya ukatili wa kingono
kwa watoto ikiwa ni tatizo kubwa linalowakabili watoto katika malezi na makuzi
yao nchini.
Hayo yamebainika mkoani Iringa wakati wa ziara ya
Naibu Waziri wa Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile alipotembelea vikundi vya malezi kwa watoto katika kijiji cha
Kising’a kilichopo Wilaya ya iirnga mkoani Iringa.
Akitoa taarifa hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii
kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Saida Mgeni amesema kuwa mkoa wa
Iringa unakabiliwa na matatizo mbalimbali na umekuwa ukiongoza katika masuala
mabalimbali yasiyofaaa katika jamii ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Ameongeza kuwa Serikali ya mkoa wa Iringa
imejipanga katika kuhakikisha inapambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia
dhidi ya wanawake na watoto mkoani humo kwa kuhakikisha inaratibu utoaji wa
elimu kwa wananchi juu ya madhara ya vitendo hivyo kwa wanawake na watoto.
Akizungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri wa
Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
amesema kuwa Serikali haijalala wala kufumbia macho suala la vitendo vya ukatili
wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto bali inachukua hatua kali kwa wahusika
wa vitendo hivyo wanaobainika.
Dkt. Ndugulile amezitaka Kamati za malezi ya mtoto
mkoani Iringa na nchi nzima kuhakikisha wanatoa taarifa za vitendo vya kikatili
dhidi ya wanawake na watoto kwa kuhakikisha hawawafichi watuhumiwa na
hawamalizani kifamilia kesi za ukatil wa kijinsia.
Ameongeza kuwa ni jambo la aibu kwa Tanzania ya
viwanda kuwa na vitendo vya kikatili kutokea katika jamii zetu kwani ni kikwazo
kikubwa katika kuhakikisha jamii inajiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
“Mkiona wanajamii miongoni mwenu wanataka
kumalizana katika kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia toeni taarifa ili
tukomehse vitendo hivi visiendelee nchini” alisema Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile amewataka wazazi na walezi nchini
kuhakikisha wanakaa na kuzungumza na watoto wao na sio kuwapiga na kuwapa
adhabu zinatazosababisha kupata ukatili wa kisaikilojia ambao ni hatari kwa
malezi na makuzi yao na kuhakikisha watoto hao wanapata haki zao za msingi
zilizopo kisheria.
No comments:
Post a Comment