Baadhi ya washiriki wa mbizo za kilometa 21.
Baadhi ya washiriki wa mbizo za kilometa 21.Washiriki wa mbio za kilometa 10.
Washiriki wa mbio za kilometa 10.Washiriki wa mbio za kilometa 5.
Makamu wa Rais pamoja na viongozi mbalimbali wakimaliza mbio za hisani za CRDB Marathon.Makamu wa Rais pamoja na viongozi mbalimbali wakimaliza mbio za hisani za CRDB Marathon.Baadhi ya washiriki wa mbio za hisani za CRDB Marathon.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza na washiriki wa mbio za CRDB Marathon.
Baadhi ya washiriki wa mbio hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohammed Janabi, akizungumza na washiriki wa mbio za CRDB Marathon.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harison Mwakyembe, akizungumza na washiriki wa mbio za hisani za CRDB Marathon. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na washiriki wa mbio za hisani za CRDB Marathon. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na washiriki wa mbio za hisani za CRDB Marathon.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 200 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohammed Janabi (kulia). Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kwa wanaume akipokea zawadi yake.
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kwa upande wa wanawake.
Viongozi wakiwa meza kuu.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kushoto), pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kushiriki mbio za hisani za CRDB Marathon.
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa mbio za hisani zilizokusanya zaidi ya Sh. Milioni 200 zitakazosaidia kulipa gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto 100 wanaotibiwa kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuzindua mbio hizo kwa kutembea kilomita tano akisema Benki ya CRDB inunga mkono juhudi za Serikali katika kutoa huduma bora za afya kwa watoto na kuongeza uelewa kwa jamii kuhusiana na magonjwa wa moyo kwa watoto.
“Kupata huduma bora za afya ni haki ya kila binadamu, haki ambayo ni muhimu katika maendeleo hususan watoto wetu na vijana katika kukua vizuri na kuwa na afya njema,” alisema Mama Samia.
Makamu wa Rais pia aliwapongeza washiriki na makampuni yaliyohusika kuandaa CRDB Bank Marathon kwa kuungana na kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia upasuaji wa watoto, huku akiwataka watu wote kuendeleza jitihada hizo.
“Upo usemi usemao ukiokoa maisha ya mtu umeikokoa dunia, jitihada hizi zisiishie hapa, tuendelee kushirikiana na Taasisi yetu ya Moyo katika kurejesha tabasamu kwa watoto wetu,” alisisitiza.
Akitoa hotuba yake, katikati ya shangwe na nderemo za mziki, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema mbio hizo za hisani zimefanikiwa kuvuka lengo la kiwango kilicho wekwa cha Sh. milioni 200.
Nsekela alisema mbio hizo za hisani zilizokuwa na kauli mbiu ya ‘Kasi Isambazayo Tabasamu’ zimeweza kuwaunganisha washiriki kwa pamoja kuchangia fedha hizo zinazoelekezwa kwenye upasuaji wa moyo kwa watoto.
Alisema kwa muda mrefu Benki ya CRDB kupitia sera yake ya kusaidia jamii (CSR Policy) imekuwa ikiisaidia JKCI kufanya upasuaji kwa watoto ili kuongeza ushiriki wa jamii kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ikiwamo ya upatikanaji wa huduma bora afya kwa watoto.
“Benki ya CRDB imeanzisha mbio hizo za hisani ambazo zitakuwa zikifanyika kila mwaka.
“...Tunaamini michezo ina nguvu ya kuwahamasisha watu kushiriki katika mabadiliko chanya. Nifuraha kubwa sana kwetu kuona mbio hizi za hisani za CRDB Bank Marathon zinachochea mabadiliko chanya katika jamii na kuongeza ushiriki wa watu katika kutatua changamoto na kuleta maendeleo.
“….Nimefarijika kuona watu wengi wemaungana nasi katika jitihada za kusambaza tabasamu kwa watoto wetu. Mafanikio haya tusingeyafikia isipokuwa kwa kujitoa kwao. Tunawashukuru washiriki wote na makampuni yaliyoshirikiana nasi kuwezesha kufikia lengo,” aliongezea Nsekela.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe, aliipongeza Benki ya CRDB na wadau walioshiriki katika mbio hizo za hisani kwa mchango wao walioutoa kusaidia upasuaji wa moyo kwa watoto.
“Benki ya CRDB imeonyesha sio tu ni bora kwa kutoa huduma bora kwa wateja, lakini pia ipo mstari wa mbele katika kusaidia jamii kwasababu uongozi wa benki hii unaelewa taifa lolote lenye mafanikio ni lazima kuwekeza katika afya ya watoto,” alisema Dkt. Mwakyembe.
Dkt. Mwakyembe alisema Benki ya CRDB imedhihirisha kuwa wapo Watanzania ambao wanauwezo wa kuongoza taasisi kubwa nchini na kwa mafanikio makubwa huku akibainisha kuwa miaka ya nyuma mabenki mengi yalikuwa yakiendeshwa na watu kutoka nje.
“Serikali inapendezwa sana na utendaji kazi wa Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na wafanyakazi wa Benki ya CRDB kwasabubu mnafanya vizuri katika nyanja zote, katika biashara na katika kusaidia jamii kama hawa watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo,” alisema Dkt. Mwakyembe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Prof. Mohammed Janabi, alisema sasa hivi wapo watoto 500 katika orodha ya Taasisi hiyo wanaosubiria kufanyiwa upasuaji wa moyo huku wazazi na walezi wao wakishindwa kumudu gharama za matibabu.
Prof. Janabi ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuandaa mbio hizo za hisani huku akiwataka wadau wengine pia kujitokeza kusaidia.
Katika mbio hizo za hisani washiriki hao zaidi ya 3,000 walikimbia kilomita 42; 21 na 10 wakati zile za kilomita tano zikiongozwa na Mama Samia.
No comments:
Post a Comment