HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 13, 2020

Watu wawili wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kuhusika na mauaji ya mwaka 2015 mkoani Kagera

 

 

Na Lydia Lugakila, Kagera

 
Watu wawili wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba mkoani Kagera baada ya kutiwa hatiani 
kwa kuhusika na mauaji ya mauaji ya mtu mmoja katika eneo la Kitendaguro katika Manispaa ya Bukoba yaliyotokea Machi 9, 2015, huku mmoja akiachiwa huru.


Hukumu hiyo ya kesi namba 34 ya mwaka 2020 imetolewa na Jaji wa Mahakama hiyo Sam Rumanyika baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo dhidi ya watuhumiwa hao.


Akizungumza baada ya hukumu hiyo Mkurugenzi wa usimamizi wa kesi na uratibu wa upelelezi, kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Hashimu Ngole amesema Serikali imeridhishwa na maamuzi ya Mahakama ambayo yanarejesha imani ya wananchi waliokuwa wakiishi kwa wasiwasi kwa kuhofia kukatwa makoromeo.


Mwaka 2015 yaliibuka mauaji ya kukata watu makoromeo na kuzua hofu kwa wakazi kwa baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Kagera.

No comments:

Post a Comment

Pages